![]() |
![]() |
Tunapenda kuweka wazi Kuwa tukio hili halikufanywa kwa maelekezo ya kiongozi yeyote na kama Chama hatujawahi na hatuna Sera wala msimamo wa kubagua chombo chochote cha habari.
Kwa hatua za awali tunafanyia uchunguzi tukio hilo ili kuweza kubainisha Nini hasa kilitokea Katika siku hiyo na tunategemea kupata ushirikiano kutoka kwa Mwandishi husika Katika uchunguzi wetu. Tunapenda kuwahakikishia waandishi wote wa habari kuwa wataendelea kuwa salama Katika matukio yote ambayo yatakuwa yakifanywa na CHADEMA na watapata ushirikiano unaostahili.
Baada ya uchunguzi wetu kukamilika tutatoa taarifa Kamili juu ya tutakachokuwa tumebaini na hatua tutakazochukua .
Sisi tunaamini Katika uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa waandishi wa habari na haki ya kupata na kutoa habari/taarifa kuwa ni nguzo kuu katika kujenga taifa la kidemokrasia na hatimaye kufikia maendeleo ya kweli.
Imani yetu hiyo tumekuwa tukiidhihirisha kwa vitendo hadharani, mfano, CHADEMA ni taasisi ya kwanza ya kisiasa iliyotia saini na kukubaliana na *Azimio la Dar es Salaam Juu ya Uhuru wa Uhariri na Uwajibikaji* (hatuna uhakika kama ipo nyingine iliyofanya hivyo hadi sasa).
Tunapenda kutumia fursa hii kuwahakikishia wadau wote wa habari, wakiwemo waandishi, wahariri na wananchi, kuwa tutaendelea kuionesha imani hiyo kwa vitendo katika shughuli zetu zote za kisiasa.


0 comments:
Post a Comment