Posted by Williammalecela.com on Friday, July 28, 2017
 |
Februari 22, 2002 vyombo vingi vya habari duniani kote vilitawaliwa na
habari kubwa ya kuuawa kwa mfalme wa pori na mwanaume aliyeisumbua
serikali ya Angola kwa zaidi ya miaka 27
akiongoza vita vya msituni
dhidi ya vikosi vya serikali.
Jonas Malheiro Savimbi, alikuwa
mtoto wa pekee kwa baba yake Lote, aliyekuwa mfanyakazi wa reli ya
Benguela na mhubiri wa kanisa la Protestanti lililokuwa likifadhiliwa na
Wamarekani.
Pamoja na baba yake kuwa muumini wa dini kamwe Jonas hakuwa muumini, tangu utoto wake alikuwa mtukutu.
Alisoma katika shule za Kiprotestanti na Kikatoliki, lakini akiwa na
miaka 24 alipata udhamini wa kwenda kusoma Ureno ambapo alimalizia
masomo yake ya sekondari na somo la lazima la siasa huku akishindwa
kuanza kwa wakati masomo ya udaktari wa binadamu aliyotakiwa kuyachukua.
Mwaka 1966 alianzisha vuguvugu la Unita kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno.
Katika nyakati zake za awali, kabla ya kuanzisha Unita, alijiunga na
chama cha wapigania uhuru wa MPLA mwaka 1964, muda mfupi baadaye
alijiunga na chama cha FNLA.
Mwaka huohuo alipata fursa ya
kufanya ziara maalumu China na aliahidiwa kupatiwa nafasi zaidi kwa
ajili ya mafunzo ya kijeshi na misaada ya zana za kijeshi.
Hatua
hiyo ilitokana na mgongano wa kimasilahi, baada ya FNLA na MPLA kuanza
kupingana kuhusu nani anastahili kupewa nchi iwapo watapata uhuru, hivyo
muda mfupi baadaye wakoloni hao walitoa taarifa kueleza kwamba Savimbi
anapigana kwa ajili ya masilahi yao.
Hatua hiyo ilisababisha
kuungwa mkono na Marekani iliyokuwa na masilahi tofauti na MPLA
iliyoungwa mkono na Wasovieti tangu mwaka 1974 na kilijipambanua kufuata
mrengo wa Marxist-Leninst kuanzia mwaka 1977, wakati Savimbi
alijipambanua kufuata sera za Mao na kuungwa mkono na China.
Vita
baina ya MPLA na Unita hata hivyo ilikuwa na sababu nyingi za ndani na
kwa hiyo kuanza kutumiwa kama chanzo cha mvutano wakati wa vita baridi
baina ya Marekani na USSR.
Mwaka 1966 baada ya kurejea
kutoka nchini China ambako alienda kupata mafunzo ya kijeshi alirudi na
kuunda UNITA na kuanza kupambana na serikali ya kikoloni sambamba na
vyama vingine ambavyo vyote vilikuwa vikipigana kumtoa mreno.
Hapa ndipo jina la Jonas Savimbi likaanza kusikika kote duniani kutokana
na mbinu kubwa za kijeshi alizonazo huku akisapotiwa na wananchi kutoka
kabila lake la Bieno.
Huku akipata sapoti kubwa kutoka China na
baadaye Marekani, aliongoza vita vikali kwa muda wa miaka zaidi ya 20
huku akiwa ni tishio kubwa kwa Serikali ya Luanda. Kuna muda aliwahi
karibia kuipindua serikali ya Rais Dos Santos.
Akiwa na uwezo wa
kuzungumza lugha saba kiufasaha zikiwemo tatu za ndani ya bara la Afrika
na nne nje ya bara aliweza kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali
kuwaomba msaada wa zana za kivita na alifanikiwa kuwa na jeshi imara.
Aliwahi kunusurika kuuawa mara kadhaa likiwemo jaribio la Februari 1990
ambapo aliponea chupuchupu na kukimbilia nchini Marekani na kufanikiwa
kuonana na Rais Bush ambaye alimuahidi kumuongezea zana zaidi za kijeshi
na baada ya kupona alirejea nchini Angola kuendeleza mapambano.
Baada ya kunusurika kuuawa zaidi ya mara 20 na vikosi vya serikali ya
Angola huku taarifa za kuuawa kwake zikiripotiwa zaidi ya mara 15
hatimaye 22 Februari 2002 Jonas Savimbi aliuawa.
Maauaji yake
yalitokea kwenye mapigano baina ya vikosi vyake dhidi ya serikali kwenye
mto uliopo jimbo la Moxico eneo ambalo alizaliwa. Mapigano hayo ya
kushtukiza yalipangwa baada ya vibaraka kutoa siri za mahali alipo
Savimbi na baadhi ya wasaidizi wake muhimu, haikuwa kazi rahisi kumuua.
Aligundulika alipo kuwa amejificha baada ya kufanya kosa la kutumia
satellite phone na huo ndio ukawa mwisho wake. Osama alikuwa hafanyi
kosa kama hilo,ndio maana ilikuwa vigumu kubaini alikuokuwa
amejichimbia.
Kwenye shambulio hilo kali kuwahi kufanywa na
vikosi vya serikali dhidi ya kikosi cha Savimbi walifanikiwa kumpiga
risasi 15 mwilini mwake, alipigwa kichwani, kifuani na sehemu za miguuni
na aliweza kumudu na kuendeleza mapambano kwa zaidi ya saa nne kabla ya
kuishiwa damu na kuanguka chini na kufariki.
Tukio la kuuawa
kwake bado limeacha maswali mengi mpaka leo inakuwaje na aliwezaje
kuhimili kuendeleza mapambano hata baada ya kupigwa risasi 15 mwilini
mwake?
Alizikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao ya Luena na kuhudhuriwa na wapiganaji mbalimbali wa UNITA.
Mauaji yake yalimaanisha mwisho wa mapigano ya msituni nchini Angola,
Chuma kilikuwa kimeangushwa, wasaidizi wake hawakuwa na mbinu na uwezo
kama Savimbi.
Baada ya kifo chake serikali kuu ilitangaza ya kwamba hatimaye wameangusha mbuyu wa chuma uliowasumbua miaka mingi.
Wapo wanaoamini mpaka kesho kwamba Jonas Savimbi hakuwa binadamu wa
kawaida, walimuona ni binadamu wa pekee mwenye uwezo mkubwa kuliko
binadamu wa kawaida.
Wenye imani potofu walimfananisha na jini au mzimu unaotembea popote na wakati wowote bila kujali hatari iliyo mbele yake.
Hadi mauti yake yanamkuta ameacha watoto na wake wengi ambao idadi yake
haijawekwa wazi kulingana na sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa
akiishi msituni.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Jonas Savimbi ambaye
kitendo chake cha kugomea kurudiwa kwa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo na
kuamua kuingia msituni kulipelekea kuuawa kwake.
Savimbi
alifanya kosa moja kubwa alilazimisha vikosi vyake kuingia msituni
kupambana na serikali akiwa bado hajajipanga vyema, ni bora angekubali
kurudia uchaguzi dhidi ya Rais Dos Santos.
Bahati mbaya
hakulikumbuka hilo, aliwaza jambo moja tu kuingia msituni kuandaa kikosi
chake tayari kuuondoa utawala wa Dos Santos.
Aliingia msituni
kipindi ambacho tayari kikosi chake kilikuwa kimeingiliwa na vibaraka
‘spy’ kutoka ndani ya kabila lake, vibaraka hawa waliandaliwa kwa ustadi
mkubwa na ndiyo walihusika kutoa siri zote za nini kilikuwa kinaendelea
kwenye kikosi cha Savimbi.
|
0 comments:
Post a Comment