Friday, July 21, 2017

Prodyuza kutoka Wanene Entertainment, Luffa ametoa somo kwa wasanii kuhusu kufanya muziki wa live.

“Kikubwa tu ni mazoezi na kuweka sauti yako jinsi gani uiimbe katika kuperform live na watu wengi hawafanyi hicho kitu, kwa mfano unaweza ukawa unafanya mazoezi ya live band kila siku kujifunza mwenyewe kuimba na kuzoea mazingira,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.
“Kwa sababu unaweza kwenda kuperform sehemu nyingine nje ya nchi unakuta watu wanapiga live utafanyaje, kwa hiyo kitu kizuri ni kufanya muziki mzuri sio kufanya ilimradi tu,’ amesisitiza.
Luffa ametengeneza hits kama Sweet Mangi ya Nikki wa Pili, Waya ya Joh Makini, Jux & G Nako Go Low na nyinginezo kibao

0 comments:

Post a Comment