Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Madam Flora ambaye kwasasa ni mke wa Daudi Kusekwa, ametoa kitabu kinachoitwa “SIRI ZA FLORA MBASHA” ambapo kitakuwa na majibu ya maswali ya kila mwenye swali mpaka hapo alipo huku akidai kuwa ndani ya hicho kitabu ni ukweli mtupu na na hakuna alichoacha kukiandika.
Akiongea na Bongo5, Madam Flora amesema kuwa yeye na Mwanasheria walishauriana badala ya kujibu kila mtu akamshauri na kuona ni vyema wakatoa kitabu hicho ili kila mwenye swali juu ya maisha yake aweze kupata majibu ndani ya hicho kitabu.
Aidha Madam Flora amekuwa ni mtu ambae akisemwa na watu kwa hatua ya yeye kuolewa mara ya pili ambapo kwasasa ni mke wa Daudi Kusekwa, watu mbalimbali wamekuwa wakitaka kujua nini kilimsibu mpaka yeye kuchukua hatua hiyo. Ndio maana kaamua kuleta kitabu hicho ambacho kina majibu ya kila mtu mwenye maswali juu yake.
Hata hivyo Madam Flora aliongeza kuwa alivyoona watu wanapiga simu mara kwa mara akaona ni bora aweke sehemu ambazo watu watapata vitabu hivyo kwa urahisi.
0 comments:
Post a Comment