Friday, July 21, 2017

Prodyuza anayesifika kwa midundo inayosumbua masikio ya wapenda burudani Bongo, Mr T Touchez amewataka wanaosubiri majina ya watayarishaji wakongwe, P Funky Majani na Master J kuacha kutajwa  wasahau kwani wao ndiyo mizizi ya muziki wa bongo fleva.



Mr. T Touchez amesema kuwa tayari wakongwe hao walishatengeneza historia ambayo itatajwa na vizazi vyote vitakavyoingia kwenye game la muziki wa bongo.
"Marekani wapo maprodyuza wengi lakini anayetajwa kila kona ni Dr. Dre. Kwa hiyo hapa kwetu lazima tumtaje Majani na Master Jay wao wanaelewa huu muziki walipoutoa, haswa mtu kama Majani yeye alihangaika kuichimbua mizizi ya bongo fleva na akajitolea sana kwa hiyo anahistoria yake tayari" alisema Touch 
Aidha Mr. T Touchez ameongeza "Kama kuna mtu alikuwa anafikiri Majani atasahaulika wasahau. Tayari kuna Leged hivyo hata sisi tutengeneze muziki wa dunia yoyote hatuwezi kupewa jina la legend kwani kuna watu walishatutengenezea njia" aliongeza.

0 comments:

Post a Comment