Msanii wa muziki mwenye makazi yake Tabora G-Lux Conciouz ameahidi kufanya kila jitihada kufika levo za kimataifa kutokana na msoto alioupata toka mwaka 2010 alipofika kwenye jiji la Dar es salaam kukutana na Prodyuza Minyo Masonge aliyempatia msaada
Msanii huyo kinda anayesumbua sana kanda ya ziwa pamoja maeneo jirani ndani ya Tanzania na wimbo wa sio kololo amedai yeye siyo mfuasi wa kukata tamaa amedai kwamba juhudi pamoja na malengo ya kutaka kufanikiwa ndiyo vitu vilivyomfanya mpaka sasa jina lake limekuwa kubwa ndani ya kanda ya ziwa pamoja na vituo vikubwa vya redio kupiga nyimbo zake kitu ambacho aliona kama ndoto.
Pamoja na mafanikio aliyoanza kuyapata Ikiwa ni pamoja kuhojiwa na vyombo vikubwa vya habari pamoja Wasanii wakubwa walioona kitu kikubwa ndani yake, G-Lux ameweka wazi changamoto ambazo amekuwa akikutana nazo mara kwa mara kitu ambacho mwanzo kilitaka kumvunja moyo siku za kwanza.
G lux kulia akiwa upande wa kulia
"Kitendo cha kwenda studio na kukuta foleni inayosababisha nisionane na prodyuza ilitaka kunifanya niachane na muziki, lakini kama haitoshi mara kwa mara nilishinda bila kula ili nipate tu nafasi ya kurekodi. Lakini sikuwahi kujali changamoto za kutembea kwa miguu kutoka Mbezi mwisho mpaka Buguruni Malapa kumfuata prodyuza. Sijakata tamaa kwani najiona mimi ni msanii mkubwa sana kimataifa nikiipeperusha bendera y Tanzania" G Lux
Msanii huyo kwa sasa yupo chini ya uongozi wa Barn Music tawi la Tabora akishirikiana kwa karibu na produza Lisck crever ambaye ndiye alimshika mkono tangu alipogundua kipaji chake.
0 comments:
Post a Comment