Tuesday, July 4, 2017

Msanii mkongwe wa bongo fleva, Ray C amefunguka kwa kudai maendeleo yake yamechangia kwa kiasi kikubwa kwa watu kusahau kuzungumzia maisha yake aliyoyapitia ya matumizi ya dawa za kulevya hapo awali.

Ray C amebainisha hayo baada ya mashabiki zake na wananchi kiujumla kuanza kuzungumzia jinsi alivyokuwa amejiingiza kwenye sakata la utumiaji mihadarati ambayo iliyomfanya kupoteza kabisa imani kwa ndugu na marafiki zake waliyokuwa wakijitokeza kumpa msaada ili aweze kutoka katika dimbwi hilo lakini kwa mara ya kwanza ikashindikanika na ikaja kufanikiwa pale alipoamua mwenye kuacha na maisha hayo.
"I think' kwa maendeleo yangu ya sasa yanawafanya watu waone 'the difference' unajua nilipoamua kubadilika nikabadilika pamoja na kuwabadilisha mashabiki zangu kwa sababu kwenye shida na raha wameniona 'am happy' kuona kwamba 'topic' imebadilika na watu sasa hivi wanazungumzia kazi zangu ambazo zilinitambulisha kwao",alisema Ray C.
Pamoja na hayo, Ray C amendelea kwa kusema "kwa muda niliyopoteza siwezi tena kujihusisha na mapenzi sasa hivi akili yangu ipo kwenye kazi, sioni kabisa kama nitakuja ku-share mda wangu na mtu mwingine yaani sina hata hizo 'feelings' bahati mbaya sana", alisisitiza Ray C.
Kwa upande mwingine Ray C amesema kwa upande wake haikuwa jambo gumu kurudi tena katika muziki kwa madai ya uwepo mdogo wa wasanii wa kike wenye kufanya vizuri katika kazi zao zaidi ya wanaume.

0 comments:

Post a Comment