Saturday, July 22, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemwagia sifa Profesa Kitila Mkumbo (ACT Wazalendo), kuwa ni kijana mwenye akili ndiyo sababu iliyomfanya amteue kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Rais Mgufuli amesema hayo leo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika Uwanja wa Lake Tanganyika ambapo amehutubia wananchi.
“Hongera sana Profesa Mkumbo kijana safi, sura yako ni ACTwazalendo lakini moyo wako ni ccm_tanzania. Watu wanauliza nimemteuaje mtu wa ACT -Wazalendo si nimeona ana akili ndiyo maaa nimemteua,” amesema Rais Magufuli.

0 comments:

Post a Comment