Saturday, July 29, 2017

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ray C ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Unanimaliza' amefunguka na kusema yeye anampenda sana msanii kutoka kundi la Yamoto Band, Beka Flavour na kusema anaamini atafika mbali sana. 

Ray C amesema hayo  alipokuwa kwenye 'Heshima ya Bongo Fleva' na kusema anaposikiliza wimbo wake 'Libebe' anapata kusikia muziki wa bongo fleva halisi kabisaa ambayo ilikuwa inafanywa na wasanii wakubwa miaka ya nyuma. 
"Jamani mimi nampenda sana huyu mtoto Beka Flavour, kila nikisikiliza wimbo wake ule 'Libebe' namuona mbali sana kwani kazi yake ni nzuri sana yule kijana, hakika akipata usimamizi mzuri atafika mbali mno, maana anaimba ile bongo fleva halisi kabisaa" alisema Ray C 
Beka Flavour ni msanii kutoka kundi la Yamoto Band ambaye amekuwa msanii wa pili kutoka katika kundi hilo kuachia kazi ya peke yake na kupokelewa vizuri na Watanzani, hata hivyo Beka Flavour ameahidi kuwa ataendelea kuleta kazi nzuri na hawezi kuwaangusha Watanzania. 

0 comments:

Post a Comment