Tamasha la muziki la Komaa Concert la EFM limefanyika kwa mafanikio makubwa Jumamosi hii katika viwanja vya Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameongoza maelfu ya watanzania waliojitokeza kushuhudia tamasha hilo lilikusanya watu wa rika mbalimbali.
RC Makonda amewapongeza E FM kwa maandalizi ya Tamasha hilo ambalo limewakutanisha watanzania wa hali ya chini kutoka maeneo mbalimbali ambao wamepata fursa ya kushuhudia Tamasha hilo ambalo limewahusisha wasanii mbalimbali wa vichekesho na muziki wa kizazi kipya, singeli na Hip Hop.

RC Makonda akiwa juu ya steji kuzungumza na watu waliojitokeza kwenye tamasha hilo
Katika hatua nyingine RC Makonda amewataka E FM kuendelea kuongeza masafa mikoa mingine ili watanzania wengi waendelee kuipata huduma yao iliyo bora. Wasanii ambao wamefanya show katika tamasha hilo ni Harmonize, Young Dee, Young Killer, Mwana FA, Country Boy, Aslay, Beka Flavour pamoja na wasanii wengine wa singeli.

Umati wa watu uliojitokeza kwenye show hiy

Harmonize

Ruby akifanya yake

Mwana FA

Ruby akionyesha mambo yake

Country Boy

Mwana FA akiwa na County Boy akiimba wimbo wao mpya, Turn Up

0 comments:
Post a Comment