Sunday, July 16, 2017

wiki hii kupitia mtandao wa Global Tv online, Mke wa Said Mresho (Aliyetobolewa Macho na Scorpion) alitoa tuhuma nzito kwa Mumewe huyo kuwa Kumtelekeza yeye na watoto na Kwenda kuoa Mke Mwingine.

Mke wa Said hakuishia hapo alisema pia hata mali walizopewa na wasamaria wema ameondoka nazo na kwenda nazo kwa huyo mke mpya na Kumuacha Mkewe akiwa hana Kitu. Baada ya Sekeseke hilo kuibuliwa, leo kupitia kipindi cha Leo tena cha Clouds Fm, Said Amehojiwa na Kufunguka Mazito kuhusu Mke wake Huyo

“Mke wangu nimemuacha sababu ya tabia zake mwanzoni nikiwa naona alikuwa akinisaliti lakini hata sasa anaendelea kunisaliti. Siku moja aliniomba simu akaniambia anaomba simu ampigie mtu aliyemkopesha Pesa hospitali. Nilimpatia simu mama dee na akatoka lakini alichelewa kurudi nikamuuliza vipi akasema alikuwa hapatikani lakini baadaye nikabonyeza button ya kupiga.

Nilipopiga simu akapokea mwanaume mwingine nikamuuliza vipi akaniambia huyu ni mke wake kivipi wakati ni mke wangu mimi. Japokuwa nimepata zile bajaji huwezi kuamini navyonyanyasika kwenye familia yao hata hesabu za siku hawaleti”

0 comments:

Post a Comment