
Muuza nyago kwenye video za Kibongo, Sasha Kassim.
MUUZA nyago kwenye video za Kibongo, Sasha Kassim, amevunja ukimya na kudai kwamba, yupo tayari kuolewa na msanii wa Bongo Fleva, Athuman Omary ‘Harmorapa’ kama ataamua.

Msanii wa Bongo Fleva, Athuman Omary ‘Harmorapa’.
Akizungumza na 3-Tamu, Sasha alifunguka ya moyoni kuwa, yupo tayari kuolewa na Harmorapa ambaye hivi karibuni alidaiwa kuwa ana uhusiano naye wa kimapenzi.
“Nipo tayari kuolewa na Harmorapa kama akiridhia, sioni ajabu yoyote kwa sababu ni mwanaume rijali kama walivyo wanaume wengine,” alisema Sasha.
0 comments:
Post a Comment