“Nilikuwa nafuatilia baadhi ya post ambazo alikuwa anapest kipindi cha nyuma akilalamika kuhusu ugonjwa uliokuwa unamsumbua ambao alikuwa nao zaidi ya miaka 10 anahangaika na akasema kuwa hawezi kuzaa kutokana na hilo tatizo.
“Uanamke kuwa na mtoto ndio unaona vile umekamilika kuwa mwanamke au kuitwa mama unaona raha sana…ni furaha ambayo huwezi kuielezea.
“Kwa hiyo, leo nilivyoamka na kuona ile post, amepost na ameshika mtoto Mungu anatenda, Mungu akiamua anafanya. Nilifurahi sana kuona Happiness leo hii mtu aliyekuwa analalamika kwamba hawezi kubeba mimba, ana matatizo zaidi ya miaka 10 leo hii amemshika mtoto wake.” – Shamsa Ford.
Kwa upande wake Shilole ameelezea hisia zake akisema kwamba hakuna mwanamke ambaye hapendi kuzaa au kuitwa mama lakini mara nyingi suala la mtoto ni mipango ya Mungu.
“Mimi kama mwanamke na mama mwenye watoto nilishawahi kumsikia Magese na tatizo lake la kutopata mtoto, anavyokuwa analia tatizo lake la kutopata ujauzito.
“Hakuna mwanamke asiyependa kupata mtoto, hakuna mwanamke asiyependa kuzaa ila inatokea tu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Nimefurahi kuona amepata mtoto kwa mara ya kwanza na ndiyo mtoto wake wa kwanza, Mungu ambariki.” – Shilole
0 comments:
Post a Comment