Posted by Williammalecela.com on Monday, July 31, 2017
 |
Golikipa wa kimataifa wa Tanzania Aishi Salum Manula kesho tarehe
moja,anatarajiwa kujiunga rasimi na kambi ya klabu yetu ya Simba iliopo
Eden Vale Johannesburg, nchini Afrika kusini. Manula ambae ndio
Golikipa namba moja wa nchi hii ameshamalizana kila kitu kuhusu kujiunga
na klabu yetu,na ameahidi kuwapa furaha wanachama na washabiki wetu,sambamba na kuisaidia klabu kushinda mataji itakayowania msimu huu.
Wakati huo huo kesho timu ya Simba inatarajiwa kucheza mechi ya kwanza
ya maandalizi ya msimu dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika Orlando
Pirates ya nchini Afrika kusini. Orlando ambayo ndio klabu maarufu
zaid nchini humo,imeahidi kushusha silaha zake zote muhimu ili kuwapa
maandalizi ya kutosha Simba,Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye dimba
la Orlando liliopo jijini Johannesburg. Mechi nyingine ya mwisho
itakayochezwa na Simba nchini humo itapigwa siku ya Alhamis ya wiki hii
dhidi ya mabingwa wa soka nchini humo kwa sasa Bidvest *Mwisho*
klabu ya Simba kesho inawaalika waandishi wa habari kwenye mkutano wake
utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Kilenga uliopo jengo la New
Millenium,mkabala na kijiji cha Makumbusho,Kijitonyama hapa jijini Dar
es salaam Mkutano huo kwa waandishi tu,unatarajiwa kuanza saa Nne na nusu asubuhi. IMETOLEWA NA... *HAJI MANARA*
MKUU WA HABARI WA SIMBA *SIMBA NGUVU MOJA*
|
0 comments:
Post a Comment