Tuesday, July 4, 2017

Tamasha kubwa na maarufu zaidi la muziki barani Ulaya lijulikanalo kama, Roskilde festival ambalo hufanyika jijini Roskilde nchini Denmark mwaka huu limehitimishwa na mashindano mafupi ya mbio za utupu yajulikanayo kama (The Naked Run) ambapo washindi wawili wa mbio hizo wameshinda tiketi za kuingia bure kwenye tamasha hilo mwakani .
Tamasha la Roskilde festival lilianzishwa mwaka 1971 na hufanyika kila mwaka kwa kuwaleta Wasanii wakubwa kutoka Marekani na Ulaya, mwaka huu limehitimishwa kwa kusindikizwa na shindano la The naked run ambalo kwa kawaida hufanyika jumamosi ya kwanza ya mwezi Julai kila mwaka nchini Denmark.Kwa mujibu wa Mtandao wa Tamasha hilo umeeleza kuwa mbio hizo za utupu ambazo hufanyika Jumamosi ya kwanza ya mwezi Julai hugongana siku na Tamasha la Roskilde festival hivyo wameamua kuunganisha mashindano hayo ya kukimbia utupu na Tamasha lao ili kuongeza idadi ya watazamaji.Tangia yalipoanzishwa mashindano hayo ya The Naked Run mwaka 1999 nchini Denmark yanafanyika kwenye miji mikubwa nchini humo kila mwaka isipokuwa Copenhagen kwa sababu za kiusalama.
Tamasha la Roskilde festival mwaka huu lilianza june 24 na kumalizika wikiendi iliyopita julai 1 na limehudhuriwa na zaidi ya watu laki moja na kiingilio kilikuwa ni Euro 225 kwa mtu mmoja na huduma zote ni juu yako kwa wiki nzima.
Wasanii wakubwa waliohudhuria mwaka huu ni Ice Cube, Young M.A, Gucci Mane na Solange na wasanii wengine 130 .

They didn't want me to leave!  Wow this is a blessing 2 be in Denmark  a place I would never imagined to perform at Thank You!!!




Tazama baadhi ya picha zinazoonesha washiriki wa mbio hizo za utupu ambao walikuwa washiriki 30 Wanaume kwa Wanawake na muonekano wa majukwaa ya tamasha lote.



Young M.A akitumbuiza kwenye Tamasha hilo
Gucci Mane

Baadhi ya washiriki wa mbio hizo wakishindana kwenye tamasha hilo


Washiriki wakiwapongeza washindi wa mbio hizo

Wahudhuriaji wa tamasha hilo wakitazama mbio hizo za maajabu

Moja ya mshiriki aliyeibuka kidedea kwenye mbio hizo
Hawa ndiyo washindi wa mbio hizo watakaoingia kwenye tamasha hilo mwakani bure na kupata kila huduma kwa wiki nzima kuanzia June 30 hadi Julai 7 – 2018

0 comments:

Post a Comment