Sunday, July 30, 2017

Huwezi kuwataja female rappers wanaofanya poa kinoma hivi sasa kwenye game ya music East Africa ukaacha kumtaja mwanadada Rosa Ree zao la The Industry, kutokana na hits ambazo anadropisha back to back, juhudi zake kwenye game na mambo mengine kibao.

 Rosa Ree amekamata kutusanua kitu kingine ambacho huenda angekuwa anafanya tofauti na kuwa msanii kama ambavyo wengi tunamfahamu.
Rosa Ree ametusanua kuwa tofauti na muziki huenda angekuwa daktari, kutokana na chaguo ambalo alikuwa amelifanya hapo awali baada ya kumaliza kidato cha sita na kuitaka familia yake iwekeze nguvu zake katika kumpa sapoti katika sekta hiyo.
Rosa amedai kwamba alisoma kabisa masomo ya udaktari ila mwisho wa siku aliamua kuachana na harakati hizo na kuamua kufanya kile kitu ambacho anapenda (Music) na wala haikuwa shida kwa familia yake kuweza kukubaliana naye na kumpa sapoti.

0 comments:

Post a Comment