Mfanyabiasha Ramadhani Athumani Juma maarufu kama Elias Jeremiah Mazimbaka amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kujitambulisha kuwa yeye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa.
Wakili wa Serikali, Jacqline Nyantori amedai kuwa kati ya Juni 28 na Julai 4, 2017 jijini Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya alijitambulisha kama Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu kwa Ladslaus Matindi.
Amedai kuwa mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo katika kipindi hicho kwa lengo la kujaribu kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu
Mshtakiwa amekana shtaka ambapo upande wa mashtaka ulidai upelezi bado haujakamilika na Mshtakiwa ametakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya shilingi milioni 1 milioni.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 23 mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment