![]() |
| Leo Balozi Wa Ujerumani Tanzania Balozi Dr. Detlef Wächter amekabidhi
jengo litalotumika kama makazi na kufanyia Kazi ya ulinzi na usalama
kwenye mbuga ya Serengeti . Makabidhiano hayo yamefanyika Fort Ikoma,ambapo jengo hilo lililojengwa kwa ufadhili Wa Benki ya maendeleo ya KfW ya Ujerumani limekabidhiwa kwa Serikali na limepokelewa na Mhe.Prof. Maghembe Jumanne Waziri Wa maliasiri na utalii Tanzania. Kwa namna ya kipekee kabisa hii Ni hatua muhimu itakayoondoa visingizio kwa baadhi ya watendaji kwa maana jengo hilo litakuwa na vifaa vya kisasa na madhubuti katika kuhakikisha wanyama wetu na maliasiri iliyomo Serengeti inatunzwa kwa Faida ya kizazi hiki na kijacho Katika nchi yetu sekta ya maliasili inasimamia wanyapori,misitu ,ufugaji Nyuki ,malikale na utalii ambapo maeneo yaliyohifadhiwa kisheria yanahusisha misitu ya hifadhi na mbuga za wanyapori ambayo yanafikia takribani hekta milioni 28 sawa na 33% ya ardhi ya Tanzania na katika mbuga za wanyamapori inayoongoza Ni Serengeti Mbuga ya Serengeti umekuwa muhanga mkubwa Wa majangiri na uvamizi Wa mifugo ambao umekuwa ukiongezeka kwa kasi licha ya kuwepo kwa sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009(sura namba 283) Hata hivyo pamoja na wizara kuwa na Magari zaidi ya 24,pikipiki zaidi ya 30,GPS zaidi ya 50,genereta 50 ,Ndege zisizo na rubani(UAV's), Ndege ndogo aina ya Husky ,pamoja na kuendelea kuwaongezea wafanyakazi ujuzi Wa kukabiliana na vihatarishi vya hifadhi na mbuga, jengo hili litaongeza chachu katika kuhakikisha mbuga ya Serengeti inakuwa mahali salama pa kuishi Simba,Chui,Vifaru,tembo,pundamilia,nyati,nyani,swala,tumbili na bila kusahau Nyumbu. |
![]() |
![]() |



0 comments:
Post a Comment