
Jeshi la polisi nchini
Malawi limesema kuwa limepewa kibali maalum cha kumkamata Rais wa zamani
wa nchi hiyo, Joyce Banda kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na
utakatishaji fedha.
Jeshi hilo limeeleza
kuwa limekusanya vielelezo vya kutosha vinavyoonesha kuwa Rais huyo wa
zamani ni mhusika katika kashfa kubwa ya rushwa na utakatishaji fedha
kiasi cha dola za kimarekani milioni mia mbili na hamsini ($250m),
katika kashfa inayofahamika kwa jina la ‘cashgate scandal’.
“Jeshi la polisi la
Malawi linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa kitengo chake cha kupambana
na rushwa na udanganyifu kimefanya uchunguzi kuhusu tuhuma dhidi ya
Rais Mstaafu, Joyce Banda na kimepata vielelezo vya kuaminika,” imeeleza sehemu ya taarifa ya polisi kwa umma.
“Vielelezo
vilivyokusanywa vinaweza kuonesha kuwa Rais Mstaafu alifanya makosa
yanayohusu matumizi mabaya ya ofisi na utakatishaji fedha,” aliongeza.
Mama Banda yuko nje ya
nchi hiyo lakini polisi wamesema kuwa watatumia mfumo wa polisi wa
kimataifa (Interpol) kusaidia kumrejesha nyumbani ili ajibu tuhuma hizo
dhidi yake.
‘cashgate scandal’ ni kashfa kubwa ya rushwa kuwahi kutokea katika historia ya Malawi inayohusisha vigogo wa serikali.

0 comments:
Post a Comment