Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC), Prof. Mohammed Janab
ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kuwa moyo wa Mfanyiabiashara
Yusuf Manji umewekwa vyuma ili kumsaidia kupumua.
Prof.
Janab ambaye ni Daktari wa moyo ambaye ni Shahidi wa kwanza wa upande wa utetezi ameyasema hayo mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati akitoa ushahidi katika kesi ya dawa
za kulevya inayomkabili Manji ambapo akiongozwa na Wakili wa utetezi,
Hajra Mungula, alisema yeye ni Daktari wa moyo wa Taasisi ya JKIC.
Amesema
anamfahamu Manji baada ya kufikishwa katika Taasisi hiyo February 2017 akiwa
mwenye matatizo ya moyo na kuongeza kuwa alipofikishwa hapo alifanyiwa
vipimo na jopo la madaktari lililobaini Moyo wake umewekewa vyuma ambapo
akaingizwa mipira maalum na kubaini kwamba upo katika hali nzuri.
Prof.
Janab amesema alivyorudi hapo walimpokea kama mgonjwa aliyetibiwa nje ya nchi
na ripoti ilionyesha ametibiwa Florida, Marekani.
Alipoulizwa
na Wakili Mungula kama mgonjwa aliyewekewa vyuma katika moyo anaweza kutumia
dawa za kulevya, Prof. Janab alijibu kwamba huwa haruhusiwi kufanya baadhi ya
mambo ikiwemo kuvuta sigara, kutumia Heroin hivyo akitumia athari zake ni
kwamba mirija ya moyo uziba jambo linaloweza kusababisha kufanyiwa kwa upasuaji
mkubwa.
Prof.
Janab ameongeza kuwa katika awamu ya pili ya Manji kurudi hospitalini hapo
walimsaidia kumtibia maumivu aliyokuwa nayo kwa kumpa Drip ya Paracetamol’s na
Sindano ya Tram a do.
Akijibu
hoja ya Wakili wa Serikali, Timony Vitalis kwamba matumizi ya dawa za kulevya
yanaweza kusababisha ugonjwa wa moyo, Prof. Janab alijibu ndio.
Kesi
imeahirishwa hadi August 31, 2017 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi. |
0 comments:
Post a Comment