Wednesday, August 16, 2017



TAARIFA YA AWALI KUINGUA SOKO L SIDO
Natoa pole kwa wote walioathirika na janga la moto kwa wafanyabiashara soko la Sido. Soko la sido lilianza kuungua saa 21.32 Hrs jana usiku na kuteketeza mali za wafanyabiashara wa soko la sido

Pamoja na kutoa pole niwashukuru wananchi, vyombo vya ulinzi kwa ushirikiano na kazi kubwa YA kudhibiti moto usiendelee kuleta madhara makubwa zaidi
Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Mbeya imeunda kamati ya kufanya tathmini ya kujua hasara na chanzo cha Moto huo
Tunaomba wananchi waendelee kuwa watulivu na watoe ushirikiano kwa kamati hiyo ili tuweze kujua chanzo cha moto na hasara iliyopatikana
 
Aidha vyombo vya ulinzi vinaendelea kuchunguza kujua kama moto huo utakuwa umesababishwa na mtu/ watu uchunguzi huo bado unaendelea. Nirudie tena kuwapa pole wote walioathirika na janga na mungu awatie nguvu ktk kipindi hiki Kigumu
 
Amos G.Makalla


0 comments:

Post a Comment