Friday, August 4, 2017

19c2baeb8a97652242f91e73f50bf020.jpeg

=> Polisi wamefika Nyumbani kwa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche,
sasa Hivi wa naomba kuchukua simu zake zote na wanamueleze Kuwa anatuhumiwa kwa kuchochea wananchi kuvamia Mgodi na yupo chini ya Ulinzi. Kosa la Pili analotuhumiwa nalo ni Kuhamasisha Kilimo cha bangi. Alipokuwa kwenye Mkutano wa hadhara Silali, aliwaambia wananchi kwamba atapeleka Hoja binafsi bungeni ili bangi iwe zao la Biashara.

=> Polisi Wamechukua simu moja na Ipad ila kakataa kuwapa Password.

1-27.jpg => Vilevile Polisi Wamemtaka Esther Matiko Mbunge wa CHADEMA Tarime Mjini, Kujisalimisha Polisi aunganishwe kwenye kesi ya Heche kwani na yeye alikuwepo kwenye Mkutano wa Silali.
  

0 comments:

Post a Comment