Chama
Cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad kmepata pigo jingine kufuatia Mahakama Kuu nchini Tanzania
kutupilia mbali pingamizi lao kutaka Profesa Ibrahim Lipumba asipewe
ruzuku za chama hicho.
Mahakama
Kuu imetupilia mbali pingamizi hilo leo tarehe 11 Agosti 2017, kufuatia
Chama Cha CUF huko nyuma kufungua kesi ya msingi ya madai kuhusu wizi
wa ruzuku na shauri dogo la kuweka zuio kutolewa kwa ruzuku ya chama
kutokana na wizi wa shilingi milioni 369 ambazo zilidaiwa kuibwa na
Lipumba na kundi lake kwa kushirikiana na Msajili wa Vyama Vya Siasa.
Pingamizi
hilo limedumu kwa miezi minne kutoka Machi mwaka huu mpaka Agosti
ambapo leo Mahakama Kuu imetupilia mbali zuio hilo lililowekwa na CUF
upande wa Katibu Mkuu, hali ambayo inapelekea Msajili wa Vyama vya Siasa
kuendelea kutoa ruzuku ya Chama hicho kwa Mwenyekiti wa CUF
anayetambuliwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa. Ibrahi
Lipumba na wananchama wake ambao wanamuunga mkono.
Toka
mwezi wa Septemba 24, 2016 baada ya Profesa Lipumba kudaiwa kufanya
uvamizi wa ofisi za chama cha CUF pale Buguruni kinyume na sheria na
taratibu baada ya Kujiuzulu kwa hiari yake na kuiacha ofisi hiyo
takribani kwa kipindi cha mwaka mzima ndipo ulipoanza mgogoro kati ya
pande mbili, upande unaomuunga mkono Lipumba na upande unaomuunga mkono
Maarim Seif jambo ambalo limesababisha madhara mengi ya moja kwa moja
ndani ya chama hicho.
0 comments:
Post a Comment