Sunday, August 27, 2017

Producer Daxo kutoka MJ Records, Daxo Chali amesema hajawahi na hana mpango wowote wa kutoka kimapenzi na msanii yeyote ambaye ana msimamia chini label hiyo.

Daxo ambaye amekuwa akisimamia wasanii wa kike pekee wakiwemo Haitham na Nini, ameiambia E-Newz ya EATV kuwa  ameamua kusimamia wasanii wa kike kwa sababu wapo wachache katika Bongo Flava na si vinginevyo.
“Tanzania wapo wasanii wengi wa kiume wengi, hivyo nimetoa fursa kwa kuangalia wasanii wa kike wapo wachache  nikasema nikianza kusimamia wasanii nianzane na hawa nilete challenge na ukicheki imetokea kweli. Haitham alipotoa Fulani alikuwa ni video queen kipindi kile, so video queen wote wakanza kuimba, hiyo ni impact ambayo nimeifanya watu wengine hawawezi kuona” amesema Daxo Chali.
Hata  hivyo Daxo amesema kuwa akiona wasanii hao wamepiga hatua kubwa kiasi cha kumridhisha ataanza kusimamia wasanii wa kiume.
Alipoulizwa iwapo kuna uweli wowote wa kutoka kimapenzi na msanii yeyote miongoni mwa wale anaowasimamia alisema hiyo ni changamoto ambayo amekuwa akikutana nayo kwa sababu anasimamia wasanii wa kike pekee ila hakuna ukweli wowote.
“Kila mtu anatengeneza picha yake na kila muda nipo karibu nao kuhakikisha hawa wanafika level fulani, sasa ule ukaribu unanigharimu, lakini kiukweli mimi nawaheshimu kwa sababu tushakuwa na wasanii baadhi na tunajua matatizo ya ku-date na wasanii kwa kuangalia records label nyingine,” amesema Daxo.
Daxo anamsimamia Haitham ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Play Boy’ na Nini ambaye ana ngoma mpya ‘Kumsahau’. Kwa miezi ya hivi karibuni Daxo ametengeneza hit kama Hela ya Madee, Ukivaaje Unapendeza ya Dogo Janja na kwa sasa anajivunia ngoma mpya ya Bill Nass ‘Sina Jambo’.

0 comments:

Post a Comment