Posted by Williammalecela.com on Wednesday, August 02, 2017
 |
Baada ya taarifa ya Kifo cha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano wa Tume ya Uchaguzi nchini
Kenya IECB Bwana
Chris Musando kutokea jana niliweza kujiridhisha ‘ Kitaarifa ‘ zaidi
kutoka kwa ‘ Wadau ‘ mbalimbali wa Kenya ambao baadhi yao wanahusika
moja kwa moja ya masuala ya Uchaguzi Mkuu ujao huku wengine wakiwa ni ‘
Wabobezi ‘ wa Investigative Journalism huko Kenya ambapo kwa pamoja
walinithibitishia mambo makubwa saba ( 7 ) yaliyopelekea
Kifo hiko cha ‘
Kikatili ‘ kabisa.
Yafuatayo ni matukio ambayo Marehemu aliyafanya siku nne ( 4 ) tu
zilizopita kabla ya hayo ‘ Mauaji ‘ yake ya ‘ Kikatili ‘ kutokea hivyo
nitayaweka hapa kwenu ili kila mmoja ayaangalie na ayafanyie ‘ tathmini ‘
mwenyewe ‘ Kimoyomoyo ‘ kisha mwishoni wote tutajua ni nani ‘ Kamuua ‘
Marehemu Chris Msando.
Tukio #1.
Kwa niaba ya Tume nzima ya IECB Marehemu alipeleka ombi Serikalini la
kupewa Ulinzi wa Yeye na wenzake wote lakini hadi mauti yanamkuta
hakujibiwa wakati alipopeleka maombi ya mengine yahusuyo ufanikishaji wa
‘ Oparesheni ‘ za IECB alijibiwa na kupewa ‘ Ushirikiano haraka sana.
Tukio #2.
Siku tatu kabla ya Kifo chake Marehemu alikwenda Police kupeleka taarifa
za Yeye ‘ Kutishiwa ‘ maisha na Watu asiowajua lakini hakuna ‘ Ulinzi ‘
aliopewa hadi Umauti yanamkuta hiyo jana.
Tukio #3.
Marehemu huko nyuma alishapewa ‘ Onyo ‘ kali la kutozungumza na Chombo
chochote cha Habari nchini Kenya na ‘ Mamlaka ‘ na kuambiwa kwamba Mtu
pekee ambaye angetakiwa kuzungumza na Media basi ni Waziri tu husika wa
Habari na Mawasiliano.
Tukio #4.
Siku mbili tu kabla ya Kifo chake Marehemu Msando ‘ alikaidi ‘ hiyo amri
kutoka katika ‘ Mamlaka ‘ ambapo alikubali mualiko wa kwenda kufanya
interview na Kituo Kimoja cha Television nchini Kenya ambapo aliyoyasema
huko inasemekana kuwa ndiyo yaliharakisha ‘ mauaji ‘ yake.
Tukio #5.
Wakati akiwa ‘ mubashara ‘ kabisa akizungumza katika hicho Chombo cha
Habari Marehemu alisikika ‘ akiwahakikishia ‘ Wakenya wote kuwa kwa
jinsi alivyotengeneza ‘ Mfumo ‘ wa Kimawasiliano wa Tume ya Uchaguzi ya
Kenya ya IECB hakuna Mtu yeyote yule atakayeweza ‘ Kuudukua ‘ hata iweje
na akaenda mbele kusema kwamba Mtu akitaka ku ‘ hack ‘ taarifa zozote
za Tume ya Uchaguzi IECB basi labda akatwe ‘ Kiganja ‘ chake kwani ili
upate taarifa zao ni mpaka Yeye ( Marehemu ) atumie ‘ Kiganja ‘ chake
cha Mkono ndipo Mtu mwingine apate taarifa za Tume.
Tukio #6.
Marehemu bila kujua mbinu za ‘ Kimafia ‘ na labda pengine alijisahau
kuwa siku zote ukitaka tu ‘ Kuuawa ‘ Kimafia basi Mtu wako wa Karibu
sana ama Nduguyo au Mpenzi wako au Rafiki yako tu wa karibu ndiyo
hutumika sana kukumaliza. Marehemu usiku kabla hajafariki alifuatwa na ‘
Mwanamke ‘ ambaye inasemekana anamuamini sana ndipo huyo ‘ Mwanamke ‘
kwakuwa tayari alishapewa maagizo yote ya ‘ Kimafia ‘ ndipo akamtega
Marehemu kuwa wapite barabara fulani ambapo kumbe huko mbele ‘ Wauaji ‘
wake wale ‘ Mafia ‘ walikuwepo.
Tukio #7.
Ili kuonyesha kuwa ama hakika ‘ Wauaji ‘ wake wa ‘ Kimafia ‘
walichukizwa na Kitendo cha Marehemu kwenda mbele ya Media na kusema
kwamba safari hii katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya hakuna ‘ Udukuzi ‘wowote
utatokea kama ilivyokuwa Uchaguzi uliopita labda akatwe Kiganja ‘ chake
ndipo hata katika ‘ mauaji ‘ yake ya juzi ‘ Kiganja ‘ chake cha Mkono
ndiyo kilikatwa na kuondoka / kuchukuliwa na hao ‘ Wauaji ‘ na kuuacha
mwili wake ukiwa na majeraha mengine shingoni, machoni na tumboni.
Na kama zilivyo Kanuni Kuu za Kimafia dunia nzima ni kwamba Yule
ambaye atakuwa kafanikisha ‘ mauaji ‘ ya Mtu fulani aliyelengwa basi ni
lazima nae pia mwishoni auawe ili kufuta ama kuondoa kabisa ushahidi
wote kitu ambacho ‘ Wauaji ‘ hawa walikifanya kwa ‘ Kumuua ‘ na Yule
Dada ( Mwanamke ) pamoja na Marehemu na hatimaye mwishoni ikawa ‘
Mission
Accomplished ‘.
Soma tu kimoyomoyo na ukishamjua ‘ Muuaji ‘ Mkuu wa Marehemu Chris
Musando basi baki nalo pia moyoni. Mwishoni jiulize tu swali kwamba ni
kwanini Marehemu alipoomba msaada wa Police hakupata ushirikiano ila
baada ya kufariki jana Police wa Kenya wameonyesha ‘ Ushirikiano ‘
mkubwa Kwake ( Maiti ) huku wakiwazuia hadi Watu wengine sasa kwenda
kuuangalia mwili wa Msando na kukataa kufanyike independent post-mortem
ambapo hata Balozi wa Marekani nchini Kenya alikuwa tayari kuigharamia
kutokana na kwamba hata wao Wamarekani ‘ wamechoka ‘ na haya mauaji ya
ghafla na ya kusikitisha yanayotokea nchini Kenya kila uchao halafu
Serikali haichukui hatua yoyote ile kuyakabili / kuyadhibiti. |
0 comments:
Post a Comment