Tuesday, August 8, 2017

Wananchi wakiwa kwenye vituo vya uchaguzi mapema alfajiri leo.
IKIWA ni Agosti 8, 2017, takribani Wakenya milioni 19 wanatarajia kupiga kura kuwachagua rais, magavana wa kaunti, wabunge, maseneta, wawakilishi wa wanawake na wawakilishi wa kata.
Vituo karibu vyote vya kupigia kura vimefunguliwa rasmi tangu saa 12: 00 alfajiri, huku wapiga kura wakijitokeza vituoni kuanzia majira ya saa 9 usiku tayari kupanga foleni kwa ajili ya uchaguzi huo.
Kwa mara nyingine, Uhuru Kenyatta wa Chama cha Jubilee na Raila Odinga wa Muungano wa Upinzani (NASA), wanaonekana kuwa na ushindani mkubwa katika kinyang’anyiro hicho. Kenyatta ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta na Odinga ni mtoto wa makamu wa rais wa kwanza Jaramogi Oginga Odinga.
Maofisa wa Tume ya Uchaguzi wakiandaa fomu kwa ajili ya uchaguzi.
Waziri awahakikishia Wakenya usalama wakipiga kura
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu hali ya usalama nchini Kenya, hasa kutokana na ushindani mkali unaoshuhudiwa kati ya wagombea urais wawili wakuu huku wananchi wao wakiwa bado wanakumbuka ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Aidha, hivi karibuni Meneja wa TEHAMA wa Tume ya Uchaguzi IEBC, Chris Musando aliuawa na watu wasiojulikana. Wakati huo Kaimu Waziri wa Usalama, Dkt. Fred Matiang’i amewahakikishia Wakenya kwamba usalama umeimarishwa.
Masanduku ya kura yakipangwa.
Wapiga kura kituo cha Odinga
Wapiga kura katika Kituo cha Shule ya Msingi ya Olympic katika Mtaa wa Kibera, Nairobi walifika mapema. Mgombea urais wa muungano wa upinzani National Super Alliance, Raila Odinga, anatarajiwa kupiga kura yake katika kituo hicho baadaye leo mchana.
Wananchi wakiwa wamepanga foleni ili kupiga kura.
Hali ilivyo Mwabungo eneo la Kwale Pwani ya Kenya
Hivi ndivyo hali ilivyo kituo cha kupigia kura cha Mwabungo kaunti ya Kwale. Hapa, watu wa jamii ya Makonde watapiga kura mara ya kwanza baada ya kutambuliwa kuwa raia wa Kenya.
Maandalizi yakiendelea vituoni.
Garissa
Shughuli ya upigaji kura imeanza katika kaunti ya Garissa, Mashariki mwa Kenya ambako usalama umeimarishwa.
Masanduku yakiwa yamepangwa.
Wapiga kura wa kwanza Kwale
Upigaji kura umeanza katika Kituo cha Wabungo, Kwale, Pwani ya Kenya na baadhi ya watu wameshamaliza kupiga kura.
Pichani ni wananchi wakipiga kura.
Wapiga kura wa kwanza Kisumu
Katika Kituo cha Aga Khan, Mjini Kisumu, wapiga kura hawa ni miongoni mwa waliokuwa wa kwanza kupiga kura kituoni hapo. Upigaji kura katika kituo cha Maktaba ya Garissa umechelewa kuanza kwa saa chache
Wananchi wakikagua majina yao kabla ya kupiga kura.
Hitilafu za kimitambo kituo cha Kibra
Mitambo ya kuwatambua wapiga kura katika Kituo cha Shule ya Olympic, Kibra imeanza kukumbwa na hitilafu. Shughuli ya upigaji kura imesimama kwa muda maafisa wa tume ya uchaguzi wakijaribu kutatua tatizo hilo. Ofisa Msimamizi wa uchaguzi kituo hicho, Aggrey Mulera amesema wanajaribu kutafuta suluhisho.
Mitambo ya kupigia kura.
Wakenya wapiga kura nchini Tanzania
Raia wa Kenya waishio nchini Tanzania wamekuwa wakipiga kura nchini Tanzania katika Jiji la Dar es Salaam na A

0 comments:

Post a Comment