Posted by Williammalecela.com on Wednesday, August 30, 2017
💐
 |
KESHO NI SIKU YA ARAFAA,MAHUJAJ WATATOKA MINNA KUELEKEA VILIMA VYA
ARAFAA NI UMBALI WA 20KM.
WATATAKIWA KUKAA HAPO MPAKA SALA YA
MAGHRIB.HAPO NDIPO ILIPOSHUKA AYA YA 3 SURAT MAIDA MUNGU AKIMWAMBIA
MTUME KWA HAKIKA LEO NDIO NIMEKUKAMILISHIENI DINI YENU ,NA NI SEHEMU
AMBAYO MTUME ALIKUA AKITOA HUTUBA ZAKE KWA MAHUJAJI,NA KAMA UJAENDA HAPO
ARAFAA BASI HAJI YAKO HAISWII.NASIE AMBAO HATUKUPATA BAHATI YA KUHIJI
YATUPASA TUFUNGE SIKU IYO AMBAYO NI KESHO. NA UJITAHIDI KUFANYA HAYA :
1)lala mapema usiku wake(Leo) 2) amka saa kumi na robo za alfajiri 3)swali rakaa 2 tahajud na rakaa moja witri na uombe wakati wa sijda 4) baadae fanya istighfaar mpaka karibu na swala ya fajri 5)jiandae na swala ya fajri ikiwezekna tawadha tena ili umwage dhambi kwa maji ya udhuu 6)Soma dua baada ya kutawadha 7)swali rakaa 2 kabla ya fajri kwani mtume s.a.w asema hizo ni bora kuliko dunia na zilioko ndani ya dunia Swali fajri na ubaki kwenye mswala mpaka usome dua za subuhi alafu soma quran mpaka jua lichomoze 8)ikifika 6:35 am swali rakaa 2 za " ishraaq" ili upate thawabu za hajj na umra 10)lala kidogo angalau kwa jisaa moja ili upate afia ya kufanya ibada nyengine Ukiamka tawadha na uswali rakaa 2 za dhuha 11)endelea kufanya dhikri , istighfaar na kusoma quran 12) soma sana hii: لا اله الا الله وحده لاشريك له ,له الملك وله الحمد وهو علي كل شيء قدير 13) swali dhuhri soma quran kidogo 14) swali asri soma adhkaar za jioni 15) soma quran kabla ya adhaan ya maghrib na endelea kuomba dua na usiwasahau waislamu wenzio kwa dua 16)muombe Allah jua la siku ya Arafah lisizame ila umeachwa huru na moto 17)ikiadhiniwa maghrib futuru na usisahau dua kwa wingi kwani dua ya anaefunga hazirudishwi |
0 comments:
Post a Comment