KIFO CHA MTEMI Mbula Mtelya Kasanda maarufu MTEMI MILAMBO!
SIMULIZI za Padre Simeon Lourdel JUU YA KIFO CHA MTEMI MILAMBO.
Father Lourdel aliishi UNYAMWEZINI tangu tarehe 5 februari 1871. ukweli ni upi?
VITA KATI KAPELA NA MIRAMBO.
Mtemi Ndwikwa Kapela II, amesimulia kuwa : Kapela alikuwa na tabia ya
kutambikia kwanza kabla ya kuanza vita, wakati anajiandaa kupigana na
Mirambo alifanya hivyo hivyo Aliwaalika « Waswezi », viongozi wa
kuomba mizimu. Aliwaalika na wakaenda kwa Kapela na kuingia katika
kijumba cha matambiko (kagondo) wakakaa humo usiku kucha wakiwa pamoja
na Kapela mwenyewe. Kulipopambazuka aliwapeleka kwenye mti uliopandwa
juu ya kaburi la watoto wake ambao walikuwa mapacha, (Kulwa na Doto).
MTEMI MIRAMBO AFANYA MATAMBIKO KABLA VITA.
Padre Simeon Lourdel wa Shirika la Mapadre Weupe (White Fathers) ambae
wakati huo alikuwa rafiki yake Mirambo, katika kitabu chake
kinachosimulia kuwa « askari wa Mirambo wakati wanacheza ngoma ya ibada
ya matambiko walikuwa wamevaa manyoya ya mbuzi mabegani, walikuwa
wakiimba « Kapela ufililie mbali, Kapela ufifilie mbali… » Walirudia
rudia maneno hayo. Mirambo alipomuaga mama yake mdogo Masele kwamba
anajiandaa kwenda kupigana na Kapela. Mama yake akamshauri kwamba «
mwanangu usiende kupigana na Kapela kwa kuwa ni mjomba wako na huko
ndiko nyumbani kwetu ».. Mirambo akamjibu « mama acha, kama
unamtetea nenda kujiunga na wachawi wenzako akina Subi » (Subi alikuwa
ni dada yake na Kapela pamoja na mama yake Mirambo – Nyakasi, na Masele
mdogo wao) Baada ya matambiko, Mtemi Mirambo na askari wake waliondoka
kwenda vitani, wakafika katika kambi yao ya huko Manguwa.
MTEMI KAPELA AFANYA MATAMBIKO KABLA VITA..
Mtemi Ndwikwa Kapela II, amesimulia kuwa : Kapela alikuwa na tabia ya
kutambikia kwanza kabla ya kuanza vita, wakati anajiandaa kupigana na
Mirambo alifanya hivyo hivyo Aliwaalika « Waswezi », viongozi wa
kuomba mizimu. Aliwaalika na wakaenda kwa Kapela na kuingia katika
kijumba cha matambiko (kagondo) wakakaa humo usiku kucha wakiwa pamoja
na Kapela mwenyewe. Kulipopambazuka aliwapeleka kwenye mti uliopandwa
juu ya kaburi la watoto wake ambao walikuwa mapacha, (Kulwa na Doto). 19
Waszezi wakazunguka mti huo huku wamevaa mavazi yao ya kutambikia
kichawani (kishingo). Pia askari walileta silaha zao na kuzisimika chini
ya mti huo. Kisha kiongozi na waswezi aliwapulizia maji
yaliyochanganywa na mtama (kafupa) kuwaombea dua la ushindi. Mtemi
Kapela wakati wa maandalizi yake ya vita alikwenda Kigoma na kupata
pembe pamoja na mkuki alivyovitumia vikiwa na dawa. Pembe hilo
alilitumia kuonyesha ishara ya hatari. Aliliweka katika mlango wa ikulu
(Luzonzo), wakati wa hatari lilikuwa likivuja damu na akilikuta linatoka
maji alijua kuwa hakuna hatari yoyote. Waswezi walitunga wimbo kulisifu
pembe hilo wakiimba : « Nalini pembe lyane nalifunya kule ma Bhuha ulu
wahaya kubuma ng’wafurani na kuloga lusalo » wimbo huo ulifahamisha sana
kwa Wanyamwezi hadI leo hii.... Mkuki na aliutumia alipokuwa
akitembelea maeneo ya vita - ulikuwa umefungiwa hirizi katika ncha za
makali yake, akikutana na adui yake ana kwa ana aliuelekea makali yake
kwa adui na huyo alikufa pale pale.
VITA
Mtemi Ndwikwa Kapela
II husimulia kuwa vita vilianza mwezi octoba mwaka 1883, na vilidumu
kwa mwaka mzima. Mtemi Mirambo alikuwa amechimba handaki lililoanzia
kijiji cha Manguwa, huko Igalula ambako ndiko kulikuwa na kambi ya
Mirambo. Tarehe 1/2/1883 majeshi ya Mirambo yakitokea upande wa
kaskazini yalikaribia ikulu ya Kapela . Kapela alipoona kuwa karibu
Ikulu yake itatekwa, akatumia mbinu na kuwaambia askari wake kuwa wapige
kelele wakisema « ndugu, tuache vita » Majeshi ya Mirambo yakaamini
kweli mjomba wake anaomba waache vita kwa kujali undugu. Kulikuwepo
jemadari wa Kapela, mtoto wa Subi alipoona mbinu hizi zinafanikiwa,
waliwasongelea askari wa Mirambo na kuanza kuwashambulia kwa bunduki.
Kulikuwepo jemadari wa Kapela, mtoto wa Subi alipoona mbinu hizi
zinafanikiwa, waliwasongelea askari wa Mirambo na kuanza kuwashambulia
kwa bunduki. Mtoto huyu wa Subi aitwaye Fuzigwalyuba, ndiye alyeanza
kufyatua risasi, na baadaye askari wa Mirambo wakabana na kumpiga risasi
na kufa. Kapela aliposikia kwamba mtoto wake amekufa, akalia na kusema «
Namala bhanhu » yaani nimemaliza watu.
Dada yake Subi akawaambia
kuwa, « kumbe wewe (KAPELA) bado ni mtoto, nyamaza, tutakapoipata maiti
yake, tutakuwa tumeshinda ». Basi majeshi ya Kapela yakafanya juu chini
yakafaulu kuipata ile maiti na kuipeleka ikulu. Palipokuwepo na wazee
wanawake ambao Kapela aliwatumia kama wachawi wake wakati wa vita, nao
ni :
Ngoboizizi, Wadumwa, Kabula Shingona. Wazee hawa walikuwa
wanaambatana na Subi kwa kazi zao za kichawi. Subi alichukua tunda la
mti uitwao mwicha – akalipakata kama mtoto na kumbembeleza na kusema «
nyamaza Mirambo », wale wazee wengine wakawa wanapiga vigelegele,
wakichukua pia dawa ambayo iliwafanya wasionekana mpaka kwenye shimo
ambalo alikuwa akilitumia Mirambo kwa mapumziko. Wakamkuta humo ndani na
kumchukua kichawi na kumpeleka kwa Kapela....
Walipomfikisha kwa
Kapela, akachinjwa mbwa mweusi na nyama yake ikachanganywa na sehemu
kidogo ya Fuzigwalyuba na kutayarishwa kitoweo. Wakati maandalizi
yanafanywa ya chakula hicho, Mirambo alikuwa kikalishwa kwenye kiti
pamoja na Kapela mjomba wake akiwa hajifahamu, Chakula kilipokuwa tayari
alipelekewa Mirambo ; na kuanza kula, mara akapata fahamu na kumuona
Kapela ana kwa ana, ndipo Subi akamwambia Mirambo « kula tu mwanangu,
hapa upo nyumbani kwa wazazi wako ». Subi akamwuliza Kapela « je una
lolote la kumwuliza huyu ndiye mpwao » Kapela akamwuliza Mirambo « Mpwa
wangu umeamua kweli kupigana vita na mimi mjombao ? » Mirambo hakujibu
neno. Na Mirambo hakupata tena akili akawa amepotewa na fahamu. Subi
akamuliza Kapela kaka yake « vipi utamfanya nini mpwao ? » Kapela
akasema « ni lazima nimuue ». Akaagiza afungwe kamba shingoni - wale
wazee « wa kike » (wanawake) wakasaidiana kuvuta ile kamba na kuifunga
juu katika boriti ya nyumba. Subi akachukua « ki-chungu » kidogo knaitwa
« shindye » na kukinga mkojo wa Mirambo na kumpa Kapela anywe kidogo.
Baadaye mwili wa Mirambo ukashushwa chini na... kichwa chake kikanyolewa
nywele. hizo nywele na mkojo vipo hadi leo hii. Huo ndio ukawa mwishao
wa Mirambo!
Baada ya Mirambo kufa, Subi pamoja na wale wazee
wawili wakaibeba maiti bila kuonekana na kuirudisha katika handaki lake,
katika sehemu inayoitwa Kundikili. Wakamlaza na kuonekana akiwa
amelala. Inasemekana kwamba kifo cha Mirambo kilikuwa cha kunyongwa
tarehe 2/12/1884, siku ya alhamisi. Mirambo akiwa amelazwa katika
handaki lake si hai tena, majeshi yake hayakufahamu bado kama amekufa ;
kesho yake asubuhi yalijiandaa kwa mashambulizi kuelekea ikulu ya
Kapela. Baada ya kuona kuwa Mirambo anachelewa kutoka, hapo ndipo mdogo
wake na Mirambo aitwaye Mpanda Chalo akatumwa na Ntinginya ili
akamwambie Mirambo waanze mashambulizi. Mpanda Chalo alipoingia katika
handaki akakuta Mirambo kisha kufa. Akapeleka habari kwa Mtemi Ntinginya
kuwa Mirambo ameshakufa. Basi hapo Mtemi Ntinginya akasema kuwa sasa
hakuna haja ya kuendelea na vita - Mungu kishaamua. Mpanda Chalo asema
kuwa : “ kwa kuwa mimi nipo vita vitaendelea tu”. Ntinginya akasema :“
sisi tulikuwa na mkataba na Mirambo wa kumsaidia lakini sio wewe,
hatukujui !”
MWISHO WA VITA VYA MIRAMBO NA KAPELA. Mara tu
baada ya kifo cha Mirambo, Watemi wote waliokuja kumsaidia Mirambo
walikusanya majeshi yao yote na kuyaamuru kurudi nyumbani. Wakati huo
Mapadre wa Shirika la Mapadre Weupe ambao walikuwa marafiki wa Mtemi
Mirambo wakiongozwa na Padre Simeon Lourdel, walifika kumletea dawa
Mirambo ya ugonjwa wa madonda ya koo. Habari za kuaminika zinasema kuwa
Mirambo alikuwa na magonjwa mengi. Padre Lourdel aliunga mkono maelezo
ya Mtemi Ntinginya wa Usongo ya kusisitisha mapigano.
...Wakateuliwa watu wa kubeba maiti ya Mirambo na kuirudisha Ulyankulu,
katika ikulu yake ya Ikonongo, kupitia Ngokolo (Iwe lya shinga),
wakaongozana pamoja na Padre. Walipofika Iwe Lya Shinga, mama yake
(mdogo) aliipokea maiti, kisha Padre akafanya ibada ya marehemu.Baadaye
maiti ikapelekwa Ushetu katika ikulu ya Mtemi Magope, iitwayo
Itulamashiki. Magope akaiosha maiti ile kuonyesha uhusiano waliokuwa nao
kati yake na Mirambo. Mara baada ya tukio hilo safari iliendelea hadi
Ulyankulu katika ikulu ya Mirambo, Ikonongo. Mrithi wa Mirambo alikuwa
mdogo wake Mpandachalo.
UTATA...
Kifo cha Mirambo katika
maelezo haya kinataufautiana na maelezo yaliyomo katika kitabu
kilichoandikwa na Padre John Kabeya. Maelezo yaliomo katika kitabu cha
Kabeya yanamwelezea Mtemi Mirambo, lakini katika maelezo haya ya Padre
Simeon Lourdel ni maelezo hasa ya Mtemi Kapela na maisha yake. Hivyo
basi haya yote yamepatikana huenda kwa sababu ya kumsifia Mtemi Kapela
na yale ya Kabeya ilikuwa kumsifia Mtemi Mirambo.
Kila upande unasimulia
sifa na ushujaa wa Mtemi anayehusika. Ni jambo la kutia moyo na kutoa
nafasi ya uchunguzi zaidi kwa wataalamu wa fani ya mambo ya kihistoria
na ya kale kutafuta maelezo sahihi ya KIFO CHA MTEMI MILAMBO
|
0 comments:
Post a Comment