Wednesday, August 2, 2017

Mwenyekiti Ana Mwenyekiti Wake, Salim Abri Asas..
Bodi ya Udhamini, Iringa International School.
Ndugu zangu,


Pichani nimesimama na Salim ' Asas' Abri kwenye moja ya visima vya kijamii shambani kwake. Ni mwaka 2013.
Salim ni jamaa yangu wa karibu hapa Iringa ninakoishi.
Na kwa ukweli, Salim ndiye aliyenifanya mimi na familia yangu tuchague kuishi Iringa, maana, kabla ya kuja Iringa kutoka Sweden, mwaka 2003 nilifika Iringa nikitokea Sweden nilikoishi kwa miaka 13. Nilikuja kuona kama kuna uwezekano wa kuja kufanya kazi hapa na kama, kubwa kabisa, kama kuna shule ambayo watoto wangu wangeweza pia kusoma. Shule yenye kutoa elimu ya viwango vyenye ubora wa Kimataifa na yenye mazingira mazuri ya kujifunzia.

Salim alikuwa Mjumbe na Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya Iringa International School. Alipofahamu kutoka kwa Mwalimu Mkuu, kuwa nimekuja kuitembelea shule hiyo, basi, Salim, kama mwenyekiti wa bodi, na hata kama hatukuwahi kukutana, alichukua jukumu la kuniandikia email kunielezea zaidi juu ya shule hiyo na hata kunishawishi, mimi na mke wangu mpenzi, kufanya maamuzi ya kuchagua Iringa na Iringa International School.

Hata hii leo, miaka kumi na nne baadae, Salim na mimi bado tunashirikiana kwenye kazi za kijamii ikiwemo kuongoza shule ya Iringa International School. Sisi wawili ndio Wajumbe wa Bodi ya Udhamini, Salim ni Mwenyekiti wangu na mie ni Makamu wake.
Watoto wetu, wa Salim na wa kwangu, wamesoma na kumaliza Iringa International School. Tunasubiri wajukuu nao waje kusoma 

Iringa International School.
Nawe unakaribishwa sana kuleta mtoto wako kwenye Iringa International School. Ni shule yenye kutoa wanafunzi bora wa viwango vya Kimataifa.
Karibu, Iringa International School!

https://www.youtube.com/watch?v=0VhQ1wUpuCw
 
Maggid,
Iringa.

0 comments:

Post a Comment