KATIKA HILI LAZIMA NISEME
NI AIBU KWETU MAWAKILI
Baada ya kutokea uharifu wa kijinga na kinyama dhidi ya ofisi za mawakili wa kampuni ya IMMA, kumekuwapo na dhana tofauti kuhusu aliyefanya na kuratibu uwendawazimu huo. Nasema dhana maana polisi wanaendelea na uchunguzi.
Kwa jinsi ninavyoifahamu kampuni hii, kuna swala liko wazi, msuguano wa kimaslahi kati ya wakurugenzi wa juu wa kampuni, Wakili Masha na Wakili Magai. Wakili Masha amekuwa akidai kuwa Mkurugenzi mwenzake kamdhurumu mamilioni ya pesa na kumweka katika hali ngumu kimaisha.
Watu wa karibu na Wakili Masha wanalijua hilo na amekuwa hafichi hisia zake kuhusu hili na tab ya Masha inajulikana sitaki kuhukumu anahusika la hasha lakini vitendo vya hasira alivyovionyesha aliposhindwa ubunge havimpi nafasi ya weledi na uvumilivu yanapomfika ama upande wa pili kuficha ukweli wa mzozo mzima. Hivyo uamuzi au maazimio ya TLS yanaweza yakawarudi wenyewe kwa kukurupuka.
Mimi kama mwanasheria na mtu ninaeifahamu fika IMMA na pia mwenye kuwafahamu vizuri sana mawakili hawa wawili waliokuwa maswahiba kwa muda mrefu kabla ya kuzikana, najisikia aibu na hasira kwa TLS na maamuzi yake kwa niaba ya mawakili wasomi wote.
Kwa akili kidogo tu utaona kuwa kuna uhusiano mkubwa wa hili tukio na bifu ya mawakili hawa wawili. Ni sinema ambayo mwisho wake tulio wengi na karibu na kampuni hii tunaujua. Wameuwawa mawakili kadhaa kwa matukio yanayohusiana na kazi zao Polisi wetu, wanahabari, hatukuona maazimio ya kukurupuka hivi. Tuna wanachama wengI wenye heshima katika jamii nafikiri ingekuwa vyema wakaombwa ushauri badala ya kumwachia huyu mwanasiasa.
Sitaki kuiona TLS ikitekwa na wanasiasa na kugeuza taaluma kuwa siasa. Sina maana tusilaani ushenzi uliofanywa bali tuwe na weledi kama wanataaluma na tujue la kusema na wakati wa kusema na siyo kujiingiza ndani ya kimbunga kabla uelekeo wake haujafahamika.
Jehi la polisi na Idara ya usalama kwa muda sasa limekuwa katika Kazia kubwa ya kusaka na kuwataka wananchi kufichua wale wenye sare za Polisi kwani kuna kuzagaa kwa sare za polisi mtaani na zinatumiwa na wahuni, baadhi ya watu wako kolokoloni kwa kuhusishwa na matukio ya sare za polisi kuzagaa mtaani nakumbuka hata The Original Comed walisha wahi kuonywa dhidi ya matumizi ya sare hizo na sijawahi kuona chama chetu kikiwasaidia polisi hata kwakulaani tu,
Nasema ni aibu kwetu kwa sababu Mwenyekiti anataja kazi chache za IMMA moja hin inayoumiza sana Immma wanawakilisha wateja mbalimbali, wanakilisha kampuni ya madini ya Acacia ambayo ina mgogoro mkubwa na serikali akiuficha ukweli juu ya Sakata la yeye na IMMA kuisaidia kampuni iliyopokonya Ndege za Tanzania kwa madeni watanzania wamepigwa butwaa Tunasaidia wanao hujumu Taifa NI AIBU MNO.
Ni aibu kwa wanasheria kusimama ukishutumu kitendo hiki na kuitaka Serikali Itoe msaada huku upande wa pili tukionekana kufurahiya na kusaidia waporaji Rasilimali za Watanzania
Ni aibu kwani Tukiwa wanasheria watanzania wajibu wetu ni upi kwa maslahi ya Taifa?
Mnataka kuuaminisha umma nini?,mnadhurumiana na kwa sasa Tulio wengi tunajua mzozo mwingine ambao IMMA
wanamshutumiana juu ya Maslahi na Ushiriki wa dhati kuwasaliti Wananchi wa Nchi hii dhidi ya Wizi wa Rasilimali za Watanzania kwavile mnatetea wateja wa kila aina ni aibu kwa Lissu unasimama kutuhubilia wakati unaujua fika mzozo wa kimaslahi wa IMMA mwenzetu ni mshirika wa karibu mno wa IMMA na una siri za mesi nyingi zinazosimamiwa na Imma dcidi ya Serikali, unajua hata Barua Namba na Kesi namba inayosimamiwa na IMMA dhidi ya Kampuni iliyoishitaki Tanzania na msaada mlioutoa kuainisha mali za Tanzania,unajua hata tarehe na Siku walipo peleka barua za Kesi kwa Shirika letu la Ndege.TUNAKUTAKA SASA UISAIDIE VYEMA IDARA YA USALAMA NA JESHI LA POLISI DHIDI YA SHAMBULIO HILO LA KIPUMBAVU NA LINALOFEDHEESHA TAALUMA HII.
WAKILI MSOMI.
0 comments:
Post a Comment