Wednesday, August 16, 2017

Image may contain: 1 person, playing a sport and outdoor
NI heri uwe samaki mdogo kwenye dimbwi dogo kuliko kuwa samaki mdogo kwenye dimbwi kubwa. Kwa usemi huu nimemuelewa Neymar hivi hayumo kwenye listi ya tatu bora kuwania mchezaji bora wa dunia? Hebu rudia kuangalia mchezo wa Barcelona na PSG utaona shughuli yake....
Nasema sasa nimemuelewa Neymar kwa nini aliamua kuondoka kwenye lile dimbwi kubwa lenye samaki wakubwa huku yeye akiwa dagaa.... Ni heri uwe samaki mdogo kwenye dimbwi dogo kuliko samaki mdogo kwenye dimbwi kubwa. Hili ni somo kubwa sa katika maisha yetu kwani kila sehemu kuna wafalme wake.... Naamini mwakani Neymar atakuwamo kwenye tatu bora ya kuwania mchezaji bora wa dunia....

0 comments:

Post a Comment