*NEEMA YA UPATIKANAJI WA MAJI YA KUTOSHA DAR ES SALAAM*
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Paul Makonda* leo amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa Maji ya kutosha kwa Wakazi wa Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo *Makonda* ametembelea Ujenzi wa *Vituo vya Usambazaji wa Maji, *Visima* pamoja na maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha na kutibu *Maji taka*.
*Makonda* amesema lengo la Serikali ya awamu ya Tano chini ya *Rais Magufuli* ni kumtua Mama Ndoo kichwani na kuhakikisha huduma ya Maji inawafikia Wananchi wote.
*Amesema* kukamilika kwa miradi ya Ujenzi wa Vituo *Vinne* vikubwa vya usambazaji wa Maji vinavyojengwa maeneo ya *Changanyikeni, Makongo, Wazo na Bunju*vitasaidia kuzalisha Maji ya kutosha na kutatua kero kwa Wananchi.
Katika ziara hiyo pia *Makonda* ametembelea Visima 10 ambavyo aliahidi kwenye *Ziara ya Dar Mpya* ambavyo Ujenzi wake umekamilika vikiwa na uwezo wa kuzalisha *Lita 16,000* kwa kila kisima ambavyo vitahudumia wakazi wa Wilaya ya Ubungo.
Aidha *Makonda* ametembelea eneo la Jangwani ambapo
kutajengwa *Mfumo wa Maji taka* utakaogharimu kiasi cha *Bilion 200* na eneo la *Kilongawima Mbezi Beach* kunakojengwa mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha *Bilion 135* chini ya ufadhili wa *Bank ya Dunia na Serikali ya Japan.*
Hata hivyo amesema bado Serikali inaendelea kufanya jitiada za kuhakikisha Wakazi wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke wanapata maji ya kutosha kupitia miradi mbalimbali inayoendelea.
Amewataka Wananchi ambao bado hawajaunganishwa na huduma ya Maji kufika Ofisi za *DAWASCO* ili waunganishiwe Maji *bila malipo* ambapo baada ya hapo watawekewa utaratibu wa malipo.

0 comments:
Post a Comment