Wednesday, August 9, 2017

Prodyuza wa muziki Bongo kutoka studio za Classic Sound, Mona Gangstar amewakumbusha wasanii na maprodyuza wenzake kuwa muziki siyo uadui hivyo ni vema kupeana nafasi.

Mona Gangstar amesema kitu ambacho kwa sasa kinawapoteza wasanii na maprodyuza ni kutopeana nafasi katika utoaji wa kazi.
“Mimi nasema tufanye muziki kwa ushirikiano, muziki siyo bifu, muziki ni kitu ambacho tunatakiwa tukifanye kwa ushirikiano ili watu waweze kufika mbali. Tupeane air time, tupeane muda wa kurelease, ukiona mwenzako kaachia wiki hii vuta gape uaichie wakati mwingine,” Mona Gangstar ameiambia Bongo5.
Mona Gangstar ameshatengeneza hit za wasanii kama Belle 9, Ben Pol, Young Killer, Nikki wa Pili, Edu Boy na wengineo kibao.

0 comments:

Post a Comment