Mkufunzi mdachi Louis Van Gaal ambaye alitimuliwa katika klabu ya Manchester United mwaka uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na Mreno Jose Mourinho. Kwa mara ya kwanza wamekutana uso kwa uso katika mkutano mkubwa wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA).
Van Gaal alikuwa akilaumiwa kipindi anafundisha Man United hali iliyopeleka matokeo mabovu na kutimuliwa huku nafasi yake ikichukuliwa na Jose Mourinho ambaye aliweza kunyakua mataji 3 msimu uliopita huku msimu huu akijiandaa kuhakikisha ananyakua ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza.
PICHA:Mstari mbele kutoka kushoto-Kulia; Ernesto Valverde, Massimiliano Allegri, Zinedine
Zidane, Jose Mourinho, Leonardo Jardim (Mstari wa nyuma kutoka kushot- Kulia):Claudio Ranieri, Eduardo Berizzo, Rafa Benitez, Louis van Gaal, Aleksander
Ceferin, Sir Alex Ferguson, Rui Vitoria, Pierluigi Collina
Mkutunao huo mkubwa umewajumuisha pia makocha wakubwa mbalimbali akiwemo kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ambaye amehudhuria kama balozi wa Makocha wa UEFA.
Mourinho akiwa miongoni mwa wahudhuriaji katika mkutano huo pamoja na Zinedine Zidane.
MAKOCHA WALIOHUDHURIA KIKAO HICHO
Massimiliano
Allegri (Juventus), Rafael Benítez (Newcastle), Eduardo Berizzo
(Sevilla), Sergio Conceicao (Porto), Unai Emery (PSG), Bruno Genesio
(Lyon), Leonardo Jardim (Monaco), Jose Mourinho (Manchester United),
Maurizio Sarri (Napoli), Ernesto Valverde (Barcelona), Rui Vitoria
(Benfica) and Zinedine Zidane (Real Madrid).
WACHEZAJI WALIOHUDHURIA KIKAO HICHO
Xabi Alonso, Deco, Leonardo, Peter Schmeichel, Clarence Seedorf, Dejan Stanković, David Trezeguet and Javier Zanetti.
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, mlinda mlango Peter Schmeichel akiwasili katika mkutano huo.
Mchezaji wa zamani wa Liverpool Fc, Real Madrid na Bayern Munich, Xabi Alonso akiongea na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika mkutano huo.
Sir Alex Ferguson anatarjiwa kuwa mwenyekiti katika mkutano huo, ajenda kubwa ni kuwapa nafasi makocha mbalimbali kutoa maoni na mitazamo yao kuhusiano na uboreshaji wa michuano mbalimbali katika bara hilo.
Huku Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin anatarajiwa kukutana na wachezaji wakongwe wakiwemo Peter
Schmeichel and Xabi Alonso kujadili masuala mbalimbali yanayowakabili wachezaji mbalimbali barani Ulaya.
Pia kikao hicho kitahusisha mijadala mizito kuhusiana na kanuni za mashindano, sheria za mchezo, utangazaji wa mpira wa miguu, elimu na shughuli za kijamii zitakazo wahusisha wanamichezo.
WENGER AINGIA MITINI KATIKA KIKAO HICHO.
Moja wapo wa makocha walioingia mitini na kutoonekana katika mkutano huo ni meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye amekuwa akihudhuria mara kwa mara katika mikutano ya UEFA.
Lakini kutoonekana kwa Wenger kumezua minong'ono mingi lakini sababu kubwa ni uelekeo wa klabu hiyo katika kukamilisha usajili wa wachezaji katika diridha hili la usajili huku nyota wake wawili Alexis Sanchez na Alex Oxlade-Chamberlain wanahusishwa kuondoka katika klabu hiyo. Huku pia Mkufunzi wa Manchester City, Pep
Guardiola naye hakuhudhuria akijikita katika dirisha la usajili kukamilisha usajili wa Alexis Sanchez.
Endelea kutembelea www.lemutuz.com kupata taarifa mbalimbali za michezo na kuangalia mechi mbalimbali brani Ulaya 'MUBASHARA'.
0 comments:
Post a Comment