Monday, August 7, 2017

Msanii wa Bongo Flava, Haitham amefichua siri ya sauti yake kusikika katika ngoma za wasanii wakubwa wa Bongo ingawa watu wengi wamekuwa hawafahamu hilo.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri  na ngoma Play Boy aliyomshirikisha Wema Sepetu,  kuwa ndani ya MJ Record anapofanya kazi zake ameweza kuingiza sauti yake katika ngoma za Godzilla, Temba, Sugu na Madee.
“Kabla ya project hizo kuna kolabo tayari nilikuwa nimeshafanya, kama Migulu Pande ya Madee, Fundi ya Temba, Kila Wakati ya Godzilla na G Nako na Freedom ya Sugu,” amesema.
Haitham hadi sasa ana nyimbo mbili ambazo ni Play Boy na Fulani aliyomshirikisha Mwana FA na ameeleza kuwa amekuwa chini ya MJ Record kwa kipindi cha miaka mitano.
“Sio kwamba wao hawakutaka kunitoa kimuziki miaka hiyo, ni kwa sababu nilikuwa mdogo, nilikuwa bado nasoma, nashiriki u-miss u-video queen na Daxo Chali aliniambia wewe kutoka kimuziki bado kwa sababu game limebana,” amesema Haitham.

0 comments:

Post a Comment