Tuesday, August 15, 2017

Msanii wa muziki Bongo, Ice Boy amedai kuwa amewahi kuwa na orodha ndefu ya wanawake aliyowahi kupita nao kimahusiano.

Ice Boy ambaye anajifananisha na rapper Tupac Shakuru amefunguka  kuwa amewahi kuwa na wanaweke wengi katika mahusiano na wengine ni watu maaarufu katika sanaa ya bongo ila hakuwahi kuwaweka hadharani.
“Nishawahi kudate na madem kibao ambao sikuwahi kaa nikawapost, wengine ni mastaa nahisi ni wengi zaidi, lakini sijawahi kaa nikawaweka wazi kwenye media kwa sababu najua si mapaparazi kibao,” amesema Ice Boy.
Pia ameongeza kuwa madai yanayotolewa kuwa na mahusiano na msichana ambaye ni wa rapper Darasa yanatokana na yeye kumposti mrembo huyo ambaye pia ni mfanyabiashara mwenzake.

0 comments:

Post a Comment