Posted by Williammalecela.com on Wednesday, August 16, 2017
 |
Msanii maarufu wa zamani Chid Benz amejikuta kwenye matatizo na Sheriaa tena baada ya kunaswa tena na madawa ya kulevya.Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya
Watu saba akiwemo Chid Benz ambaye jina lake halisi ni Rashid Makwiro wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa wa kipolisi Ilala kufuatia msako uliofanyika ambapo wamekutwa na dawa za kulevya aina ya heroine.
Hivi karibuni tu Chid Benz alikuwa ameanza kurejea katika kazi zake za
kisanii ambapo alitoa wimbo wa Q Cheif akielezea mateso aliyopitia huku
wengi wakiamini kuwa ameacha matumizi ya dawa hizo.
Aidha,
amekuwa akishiriki matamasha mbalimbali ya muziki na afya yake ilianza
kuonekana imeimarika, wengi wakifurahishwa na maendeleo hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema watuhumiwa hao
walikamatwa Agosti 12 majira ya saa 11.50 jioni wakijihusisha na uuzaji
wa dawa za kulevya. “Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha
msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha
mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu
na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”amesema
Hamduni.
Kamanda huyo alisema kwa baada ya kuwakamata vijana hao
sasa wanajikita kusaka mtandao mzima unaohusika na biashara hiyo ili
kuhakikisha hatua kali zinachukuliwa dhidi yao.
|
0 comments:
Post a Comment