Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abubakar Katwila au Q Chief, amemzungumzia msanii mwenzake Chid Benz ambaye hivi karibuni amefanya naye kazi baada ya kimya kirefu cha Chid, na kusema Chid Benz alistahili kufanya naye kazi kwani ni msanii mkali.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abubakar Katwila maarufu kama Q Chief, amemzungumzia msanii mwenzake Chid Benz ambaye hivi karibuni amefanya naye kazi baada ya kimya kirefu cha Chid, na kusema Chid Benz alistahili kufanya naye kazi kwani ni msanii mkali.
Q Chief amesema akimuangalia Chid Benz anamuona rapper mkali kama alivyokuwa Ngwea, ingawa amekutwa na matatizo ambayo anaamini atayashinda.
"Nimekuwa nikisoma coments nyingi na zinatia moyo, unajua namchukulia Rashid kama rapper makini, ana uwezo wa kumiliki jukwaa vizuri, akitoka Ngwea namuona yeye, mara ya mwisho kumuona niliona nuru, niliona mtu ambaye anataka kujisaidia, nikavuta hisia nikasema anahitaji kurudi nikamwambia Rashidi tufanye kazi", alisema Q Chief.
Pia Q Chief amesema kazi ambayo amefanya na Chid Benz ni moja ya kazi rahisi sana kwake kati ya zilizopo kwenye maktaba yake, hivyo haikumuwia vigumu kuifanya.
0 comments:
Post a Comment