Msanii
mkongwe wa vichekesho nchini Tanzania, Amir Athuman maarufu kama Mzee
Majuto amesema amegundua jambo lililopelekea kunyimwa kununuliwa trekta
na Rais mstaafu Jakaya Kikwete ni kutokana na kuomba kama mtu binafsi na
wala siyo kwa kikundi maalum
Mzee
Majuto amebainisha hayo hivi karibuni baada ya kupita takribani miaka
minne alipoomba kufanyiwa Majuto aliomba nafasi ya kuwasilisha jambo
lake kwa Rais wa awamu hiyo kwa kusema 'kama Mhe. Rais ananisikiliza,
namwomba aninunulie gari ya kulimia ili na mimi niweze kupata walau
kulima nikiwa mapumzikoni huko nyumbani, kwani ndoto yangu ni kuja
kufanya kilimo ni kiacha kazi hii ya sanaa'.
"Najua
kosa ambalo nimelifanya mpaka nimekosa trekta nililoomba kwa Rais
mstaafu Jakaya Kikwete ni kwa sababu niliomba kama mimi lakini tungeomba
kama kikundi chenye watu 10 au 15 tungeweza kusaidiwa na Mhe. kutokana
anapenda kusaidia wengi siyo mmoja mmoja", amesema Mzee Majuto.
Kwa
upande mwingine, Mzee Majuto amesema kazi yake ya sanaa imeweza
kumsaidia katika kumuinua kiuchumi tokea alipoanza mpaka leo hii huku
akijidai kuwa hana wasiwasi juu ya namna gani anapata ugali.
0 comments:
Post a Comment