Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akimuapisha Benedict Mashiba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Balozi wa Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba akila kiapo cha
uadilifu kwa Viongozi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Balozi wa
Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba mara baada ya tukio la uapisho Ikulu
jijini Dar es Salaam.



0 comments:
Post a Comment