Friday, August 18, 2017

Msanii Jacline Wolper amewataka watu waache kumsema vibaya kuhusu mahusiano yake, na kuwataka wamuige kwenye maisha.

Jackline Wolper amesema kitendo cha kumsema vibaya wakati wanaomsema hawana vigezo vya kuongea hivyo, ni ujinga na upuuzi na badala yake amewataka wamuige kwenye kutengeneza pesa, kwani ndiyo jambo la msingi kwake.
Wolper amesema suala la kuwa kwenye mahusiano na watu ambao walishamzidi umri alishawahi kufanya hivyo, lakini hakuna cha maana alichokipata zaidi ya maumivu, na kwamba sasa anaangalia amani ya moyo wake.

0 comments:

Post a Comment