Tuesday, August 29, 2017

Image result for transfer rumours

Lemutuz.com kuanzia hivi sasa itakuwa ni sehemu sahihi zaidi kwako kupata taarifa mbalimbali za michezo kutoka katika kila pande ya dunia kwa muda na wakati sahihi. Utapata tetesi zote za usajili barani Ulaya na Kuangalia michezo mbalimbali mubarashara 'LIVESTREAMING' katika simu, tablet au Computer yako.

Ungani na Lemutuz.com hapa chini kupata tetesi mbalimbali za usajili barani ulaya:- 

 Image result for chamberlain to Chelsea
Mabingwa wa Ligi Kuu  nchini Uingereza, klabu ya Chelsea wanakaribia kunasa saini ya kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, kwa pauni milioni 40 pamoja na Alex Oxlade-Chamberlain, 24 kutoka Arsenal. Klabu hiyo pia inakaribia kumuuza mshambuliaji wake Diego Costa, 28, kwenda Atletico Madrid kwa pauni milioni 30. (Sky Sports).
Image result for i Virgil van Dijk to liverpool
'Majogoo' wa Jiji la Liverpool wapo tayari kutumia pauni milioni 135 kuwasajili Virgil van Dijk na Thomas Lemar, baada ya kukamilisha usajili wa Naby Keita. Hii inakuja baada ya leo hii klabu ya Liverpool kuthibitisha kufikia makubaliano ya kumsajili Naby Keita kutoka Red Bull Leipzig ifikapo Julai mosi 2018. (Sky Sports)


 Image result for serge aurier to man united
Klabu ya Tottenham Hotspurs wanaweza kuikosa saini ya 'beki kitasa'  wa PSG Serge Aurier, 24, ambaye anataka kwenda kukipiga katika klabu ya Manchester United (SFR Sport)

 Image result for sam allardyce to crystal palace
Meneja Sam Allardyce ambaye alibwaga manyanga kuifundisha Crystal Palace huenda akarejea kuifundisha klabu hiyo endapo  Frank de Boer atafukuzwa kazi baada ya matokeo mabovu katika timu hiyo. (Daily Mail)

 Image result for coutinho saga
Baada ya sakata la muda mrefu linalomkabili Kiungo wa Liverpool FC, Philipe Coutinho anayetaka kutimkia Barcelona, leo hii daktari wa timu ya taifa ya Brazil Michael Simoni ameibuka na amesema tatizo la mgongo la kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho linasababishwa na msongo wa mawazo kuhusiana na hatma yake. (The Sun)

Mkurugenzi Mkuu wa 'Vibibi Kizee Vya Turin' Klabu ya Juventus Beppe Marotta amesema klabu yake itapanda dau jipya kumtaka kiungo wa Liverpool Emre Can, 23, mwezi Januari baada ya Klabu ya Liverpool kukataa kumuuza kiungo huyo katika dirisha la usajili la majira haya ya joto. (Premium Sport)

Klabu ya Manchester United iko katika mchakato wa kumpatia mkataba mpya beki wa kushoto Luke Shaw, 22, ambaye Meneja wa Klabu hiyo Jose Mourinho ameshaweka wazi nia ya kumjuisha beki huyo katika mipango yake msimu huu (The Sun)

 Image result for kieran gibbs to west brom
Meneja wa West Brom Albion Tony Pulis amejipanga kurejea Jijini London katika klabu ya Arsenal Fc na dau la pauni milioni 13 ili kunasa saini beki Kieran Gibbs ambaye anaonekana hayuko katika mipango ya Arsene Wenger kwa msimu huu (The Sun).

 Image result for john evans to man city
Manchester City wanapanga kuongeza dau jipya kunasa saini ya beki wa kati wa West Brom Jonny Evans, 29, baada ya dau la pauni milioni 21 kutoka kwa Leicester kukataliwa. Huku Meneja wa klabu hiyo Pep Guardiola amewela wazi mipangopo ya kumnasa beki huyo wa zamani wa Manchester United ili kuimarisha safu yake ya Ulinzi (Mirror).


Kiungo Mkabaji wa Real Madrid, Mcroatia Mateo Kovacic ameonesha nia ya kutaka kujiunga na Liverpool na kuondoka Real Madrid. (Goal.com)

Mbingwa Ligi Kuu nchini Ufaransa, AS Monaco wamekataa dau la pili kutoka Liverpool la kumtaka Thomas Lemar. AS Monaco wameweka wazi mipango yao ya kuendelea na kiungo huyo baada ya kuondokewa na nyota wake wengi (Sky Sports).

Klabu ya Swansea City wanataka kumsajili kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez, 20.  Kiungo huyo aliombwa kutojumuishwa katika kikosi ch 'Bavarians' wiki iliyopita ili kushughulikia uhamisho wake. (Wales Online)

 Image result for alexis sanchez to man city
Klabu ya Manchester City wanapanga kuibomoa klabu ya Arsenal Fc baada ya kupanda dau jingine kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28. Huku kiungo wa pembeni Raheem Starling akihusishwa katika dili hili akielekea katka klabu ya Arsenal (Goal).

Beki wa Manchester City Eliaquim Mangala, 26, huenda akajiunga na West Brom kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Jonny Evans, ukiwa ni mpango wa Mkufunzi Pep Guardiola kuimarisha safu ya Ulinzi ya klabu hiyo ambayo imesharuhusu magoli 2 katika michezo 3 mpaka sasa (ESPN).

Endelea kutembelea www.lemutuz.com kwa taarifa mbalimbali za michezo hususan tetesi za usajili barani ulaya na kutazama michezo mbalimbali 'MUBASHARA' ikiwemo Ligi Kuu zote barani Ulaya na Michuano ya Ligi Mabingwa barani Ulaya.


Categories:

0 comments:

Post a Comment