Lemutuz.com
kuanzia hivi sasa itakuwa ni sehemu sahihi zaidi kwako kupata taarifa
mbalimbali za michezo kutoka katika kila pande ya dunia kwa muda na
wakati sahihi. Utapata tetesi zote za usajili barani Ulaya na Kuangalia
michezo mbalimbali mubarashara 'LIVESTREAMING' katika simu, tablet au
Computer yako.
Ungana na Lemutuz.com hapa chini kupata tetesi mbalimbali za usajili barani ulaya siku ya leo:-

Kiungo wa Arsenal FC, Alex Oxlaid Chamberlain ameweka wazi nia yake ya kutaka kuondoka katika klabu hiyo na kuelekea katika vilabu vya Chelsea au Liverpool ambavyo vimeonyesha nia ya kumhitaji nyota huyo, huku Chamberlain akivutiwa zaidi na klabu ya Liverpool ambayo imemhakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi kuliko klabu ya Chelsea Fc ambayo imejaa nyota wengi katika nafasi anayocheza. (BBC Sport)

Manchester United wanamatumaini ya kuinasa saini ya nyota hatari wa klabu ya Real Madrid, mshambuliaji Gareth Bale baada ya nyota huyo kujiona kama hana nafasi katika kikosi cha Zinedine Zidane huku amekuwa katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na mashabiki katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania wiki iliyopita. (MARCA)

Washika bunduki wa Jiji la London, klabu ya Arsenal imekataa ofa zote kutoka katika klabu ya Manchester City kwa mshambuliaji wao Alexis Sanchez, huku Man City wakiwa tayari kutoa kitita kikubwa cha pesa pamoja na mchezaji kumnasa nyota huyo. Arsenal Fc hapo jana wamepiga chini dili hilo huku wakikataa kumuuza nyota huyo kwa gharama yoyote, ingawa Sanchez ameweka wazi mipango ya kuondoka katika klabu hiyo akisukumwa zaidi na kiu ya kushinda mataji. (BBC Sport)

Klabu ya Liverpool Fc bado wanaendelea na mipango yao ya kumnasa nyota wa Sothampton, mdachi Virgil van Dijk, ambayo ni moja ya wachezaji waliokatika orodha ya usajili katika klabu hiyo ambayo imetenga kitita cha £200m kuimarisha kikosi chao katika dirisha hili la usajili. (Daily Mail)

Mabingwa watetesi wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Chelsea wameweka mezani mzigo wa £25m kumnasa kiungo ambaye anataka kuondoka katika klabu ya Everton, Muingereza Ross Barkley. Chelsea wanataka kukamilisha dili hilo kabla dirisha la usajili katika majira ya joto halijafungwa ili kuimarisha kikosi chao. (Telegraph)

Mabingwa
wa Ligi Kuu nchini Ufaransa (League 1), A.S Monaco hapo jana
wamefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji hatari kutoka klabu ya S.S
Lazio, Msenegali mzaliwa wa Uhispania Keita Balde ambaye amesaini
mkataba utakaomfanya akipige katika klabu hiyo mpaka mwaka 2022 na
kukabidhiwa jezi namba 14 iliyokuwa ikivaliwa na Timeoue Bakayoko
aliyetimkia Chelsea mwezi uliopita. (AS Monaco)

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wa Leicester City, Riyad Mahrez lakini wawakilishi hiyo hawajavutiwa na nyota hiyo kitu kinachpelekea kuchelewa kwa dili hilo huku akikadiriwa kupatikana kwa kiasi cha £40m . (SFR Sport)

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kuinasa saini ya mdogo wake Eden Hazard, Kylian Hazard ambaye atajiunga na kikosi cha kuendeleza vipaji katika klabu hiyo, ikumbukwe Chelsea pia miaka 4 iliyopitwa ilimsajili mdogo wake Hazard ajulikanaye kama Thorgan Hazard. (Chelsea Fc)

Kiungo wa Leicester City, Muingereza Danny Drinkwater ametuma maombi ya kuuzwa katika klabu hiyo, huku akilazimisha kuuzwa kuungana na mabingwa watetezi klabu ya Chelsea. Drinkwater amekuwa akihusishwa kujiunga na mabingwa hao kwa dau la uhamisho wa £40m. (Sky Sport)
Endelea kutembelea www.lemutuz.com kwa taarifa mbalimbali za michezo hususan tetesi za usajili barani ulaya na kutazama michezo mbalimbali 'MUBASHARA' ikiwemo Ligi Kuu zote barani Ulaya na Michuano ya Ligi Mabingwa barani Ulaya.
0 comments:
Post a Comment