Posted by Williammalecela.com on Wednesday, August 02, 2017
 |
_*WADAU WAENDELEA KUUNDA MKONO JITIHADA ZA MAKONDA:*_
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam _*Paul Makonda*_ leo amepokea Jumla ya *Computer
za kisasa 100*
zenye thamani ya *Shilingi Million 210* kutoka kiwanda
cha utengenezaji wa nguo zitokanazo na pamba ya Tanzania cha *NIDA
Textile Ltd.*
_Makonda_ amesema Computer hizo atazitoa kwa Vituo
vya *Polisi 20* kwaajili ya kufungwa mfumo wa kisasa wa kuripoti
taarifa za uhalifu zilizoripotiwa kwenye Vituo vya Polisi kila siku
*(Crime Statistic Management Information System)* kupambana na uhalifu.
Faida za Mfumo ni kumsaidia Mwananchi kupata taarifa za ndugu yake
aliepotea pasipokujua yupo wapi kwa kumuangalia kwenye mfumo kama
anashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi mfumo utaonyesha taarifa zake kwa
wakati kwenye kila Kituo.
Aidha mfumo utasaidia viongozi kupata
taarifa za uhalifu zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi kwa wakati na
kupunguza uhalifu kwani taarifa zote za wahalifu zitaonekana kuanzia
ngazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo hivyo
kusaidia viongozi kufanya maamuzi.
Mfumo pia utaondoa Rushwa na
matukio ya Wananchi kubambikiziwa kesi kwani kila atakaefikishwa kituo
cha Polisi viongozi wote akiwemo Mheshiniwa Makonda atapata atajua.
Mfumo pia utamuwezesha kiongozi kujua idadi na aina ya uhalifu
unaofanyika kwa siku,eneo ambapo matukio hujirudia mara kwa mara sanjari
na mhalifu ambae matukio matukio yake ya uhalifu yamekuwa yakijirudia
maeneo mbalimbali.
_*“Tunaachana na kuandika taarifa kwenye
makaratasi na makaunta au madaftari kwenye Vituo vya Polisi ambayo baada
ya muda mfupi yanapotea na kumuacha Mwananchi hajui kesi yake imeishia
wapi, huu mfumo ni ukombozi na mwonekano mpya wa Jeshi la Polisi na hata
Wananchi wataachana na matatizo ya rushwa na watu kubambikiziwa kesi”*_
Alisema _Makonda._
Mfumo wa *CSMIS* utachukuwa taarifa za
Mhalifu kuanzia anapoingia kituo cha polisi CRO, Jina la Mhalifu, Aina
ya kesi,jina la Mpelelezi, Hakimu, Mahakama anayopelekwa na kama
amehukumiwa kulipa faini au kifungo.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Kiwanda cha *NIDA* _Bwana Mohamed Hamza_ amesema kampuni yao imeamua
kuunga mkono jitiada za Mheshimiwa Makonda katika dhamira yake ya
kufanya Mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Dar es Salaam.
|
 |
|
 |
|
 |
|
0 comments:
Post a Comment