Monday, August 7, 2017

Image result for vodacom tanzania
Imeelezwa kuwa , idadi ya watumiaji wa data imeongezeka hapa nchini kutoka milioni 3.4 hadi milioni 5.8 kwa kipindi cha miaka miwili.Kuongezeka huko kumekuja kutokana na watanzania wengi zaidi kuanza kutumia vifaa kama vile simu na kompyuta kwa ajili ya kutafuta taarifa na maarifa mbalimbali yanayopatikana kupitia mitandaoni.Akizungumza juu ya ongezeko hilo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mawasiliano ya VodacomTanzania PLC, Ian Ferrao, alisema kuwa watumiaji wa data, yaani matumizi ya intaneti kupitia simu za mkononi na kompyuta, katka kipindi cha mwaka 2014/2016, kupitia Vodacom imeongezeka kutoka watumiaji milioni 3.8 hadi watumiaji milioni 5.4; wote wakiwa watumiaji wa kudumu.Alisema kwa kutumia takwimu hizo kwa kipindi hicho kifupi, matumizi ya data yameongezeka kutoka asilimia 37 ya watumiaji wa simu hadi asilimia 44 kufikia mwaka jana.
Alieleza kuwa taarifa rasmi za Vodacom Tanzania zinaonyesha kwamba ongezeko kubwa zaidi la matumizi ya data liliongezeka katika kipindi cha mwaka 2014 na 2015 ambako ilitoka asilimia 37 hadi 43 ndani ya mwaka mmoja tu.
Ferrao alisema katika kujipanga kuongeza idadi ya watumiaji wa data,Vodacom Tanzania itaweka mambo mbalimbali yakiwamo bei rahisi kwa wateja na kuwa na kasi nzuri zaidi kuliko washindani wake.Kuna njia kuu nne ambazo Vodacom Tanzania itazitumia katika kuhakikisha kwamba tunabaki kuwa vinara katika eneo la kutoa huduma bora na za kisasa kwa wateja wetu.“
“ Kwanza ni wazi kwamba tutawekeza katika miundombinu yetu ili iendane na mahitaji ya watumiaji wa data waliopo Tanzania. Tutahakikisha watumiaji wa mtandao wetu wanapata data kwa spidi ya kuridhisha, kuwa na bei nafuu kwa wateja ndiyo mtandao wenye spidi nzuri ya internet kuliko mingine na pia kuweka sababu zitakazowafanya watu watake kutumia data zaidi,” alisema Ferrao.
Aidha Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa,Katika miaka ya mwanzoni ya matumizi ya simu hapa nchini, kampuni nyingi, ikiwamo Vodacom Tanzania PLC ilikuwa ikipata fedha nyingi kupitia wateja wao kupiga simu kwa wingi na kutumiana ujumbe mfupi wa maneno (SMS).amesema kampuni yake imeamua kujikita zaidi kuwa kinara wa teknolojia ya data hapa nchini ili kuongeza idadi ya watumiaji wa mtandao huo.

Ferrao alisema katika miaka ya karibuni, idadi ya watumiaji wa data imeongezeka hapa nchini na Vodacom imejipanga vilivyo kutumia fursa hiyo.

“Katika miaka ya karibuni, Watanzania wengi zaidi wameanza kutumia vifaa kama vile simu na kompyuta kwa ajili ya kutafuta taarifa taarifa na maarifa mbalimbali yanayopatikana kupitia mitandaoni. Kwa sasa Vodacom inaona kuna fursa kubwa ya ukuaji katika eneo hili,” alisema Mkurugenzi huyo

0 comments:

Post a Comment