
Wema Sepetu.
STAA
‘grade one’ kunako filamu Bongo, Wema Sepetu amewajibu watu
wanaoendelea kumsema kuwa hajui kuigiza kwamba, wajaribu kutupia jicho
la tatu kwenye filamu yake mpya ya Heaven Sent ambayo inatoka leo
(Ijumaa) ikiwa imetengenezwa kwa gharama ya shilingi milioni 40.
Akizungumza
na Ijumaa, Wema alisema kuwa ameamua kutumia kiasi kikubwa cha pesa ili
filamu ionekane nzuri na yenye hadhi kwa sababu filamu nyingi Bongo
zinakuwa mbaya kutokana na bajeti kuwa finyu.
“Naamini
kila mmoja anaweza kujua uwezo wangu mkubwa niliopewa na Mungu kwa
kuiangalia filamu yangu ya Heaven Sent, ndani ya filamu hiyo utanijua
vizuri ni msanii au naleta longolongo na humo nimejitupa utafikiri sio
Wema mimi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment