Wema Sepetu.
KESI inayomkabili staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu,
imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu kutokana na shahidi upande wa
serikali kutofika mahakamani kwa kile kilichoelezwa kuwa amepata
dharura.
Agosti
1, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba, shahidi
wa kwanza wa upande wa Jamhuri aliyefahamika kwa jina la Elias Mulima
kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali akisoma ripoti ya uchunguzi
alisema mahakamani hapo kuwa mkojo wa Wema baada ya kupimwa ulikutwa na
chembechembe za bangi.
Hata
hivyo, wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alisema ripoti hiyo
iliyosomwa na Mulima ina upungufu mwingi wa kisheria. Baada ya kutokea
malumbano hayo Hakimu Mkazi Simba aliwaomba mawakili wa pande zote mbili
kuridhia apate muda wa kuipitia taarifa hiyo ya Ofisi ya Mkemia Mkuu
ili itakapoendelea aweze kuitolea ufafanuzi.
Pia
mahakama hiyo imepokea maelezo ya Mkemia Mkuu na fomu iliyotakiwa
kuambatanishwa kwenye ripoti ya mkemia ya mwanzo ambayo Wakili Kibatala
alikuwa akipinga kutoambatanishwa wakati huo hakimu ameeleza kuwa haina
umuhimu.
Wema na wenzake wanashtakiwa kwa kosa la kukutwa na kutumia bangi ambapo kesi hiyo itaendelea tena Agosti 15 na 16 2017.

0 comments:
Post a Comment