Mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima amefunguka na kusema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ataishi siku zote kwa jina la Yesu na kusema anaamini watu waliofanya shambulio hilo wanamsikia hivyo awataka kutubu.
Mchungaji Gwajima amesema hayo leo alipokuwa akifanya maombezi maalum kwa ajili ya mbunge huyo aliyepigwa risasi tano mwilini mwake Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma, Gwajima anasema anaamini watu waliofanya tukio hilo wanasikiliza mahubiri yake na kuwataka kuomba msamaha.
"Tundu Lissu ana baba, ana mke na watoto anatakiwa kuishi na ataishi kwa jina la Yesu, sisemi kwa ajili ya Tundu Lissu tu bali nasema ili nchi ipone, mambo haya lazima yasemwe bila woga, tatizo linapotokea kwenye nchi hakuna anayekuwa salama, hakuna jambo baya kama kuwa kwenye nchi hujui unaelekea wapi, naamini nchi ya Tanzania itaendelea kuwa salama, hii nchi ya Mungu itaendelea kuwa salama, naamini magaidi hao wanasikiliza mahubiri yangu sasa wale wote wanaomwaga damu bila kutubu na wao yawarudie yale yale, mambo haya tunatakiwa kuyakemea bila kuangalia upande ndiyo Mungu anataka" alisisitiza Gwajima
Mbali na hilo Mchungaji Gwajima amesema kuwa mtu ambaye amemdhuru Tundu Lissu lazima itakula kwake kwani leo atafanya maombezi ya kuyarudisha aliyoyatenda kwa Mbunge huyo yamkute yeye.
"Aliyemdhuru Tundu Lissu itakula kwako, lazima tuyarudishe kwako, bwana sema naye tumrudishie maovu yake mwenyewe, sisi tunamuomba Mungu likupate lile lile unalotaka alipate mwenzako" alisema Gwajima
0 comments:
Post a Comment