LEMUTUZ

Friday, September 8, 2017

BREAKIN NEWZZ:- RAIS WA ZAMANI WA TFF NA WENZAKE WATINGA MAHAKAMA YA KISUTU TENA LEO LIVE.

Posted by Williammalecela.com on Friday, September 08, 2017
Image may contain: 4 people, people smiling, people sitting
Kesi ya Malinzi yapigwa kalenda tena
Kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake wawili imeahirishwa baada ya hakimu anayesikiliza shauri hilo kuwa na dharura hapo jana.


Wakili wa Serikali, Faraj Ngokah ameieleza Mahakama ya Hakimu Kisutu leo Alhamis, kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Wilbard Mashauri ana udhuru.
"Washtakiwa wapo Mahakamani, lakini Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri ana dharura, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili kutajwa" alidai wakili Ngokah.

Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa aliahirisha kesi hiyo September 21 mwaka huu itakapotajwa. Mbali na Malinzi, washitakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga. Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha.

Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

TOTAL PAGEVIEWS

Popular Posts

  • LIVE: RAIS MAGUFULI ANAKABIDHIWA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA MADINI
  • BREAKING NEWZ: BASI LA NGANGA LATUMBUKIA MTARONI KULIKWEPA LORI
  • THE UDAKUZ: WEMA SEPETU Vs WOLPER!!
  • IRAN NA MAREKANI WAZIDI KUIMARISHA UHUSIANO
  • PICHA YA KWANZA YA KANISA LA ASKOFU MTATA GWAJIMA BAADA YA KUKUMBWA NA BOMOA BOMOA YA SERIKALI JANA LIVE.
Copyright © LEMUTUZ

Developed by MKCT