
Juhudi za klabu ya Manchester City
kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez zilishindikana
siku ya mwisho ya dirisha la usajili baada ya Arsenal kukosa mchezaji
wa kuziba nafasi yake.
Manchester City na Arsenal walikuwa
wamefikia makubaliano, kwa masharti hata hivyo, kuhusu kuhama kwa
Sanchez, 28.
Ada ya uhamisho wake ilikuwa £55m, na
huku ikitarajiwa kufika £5m, lakini ilitegemea kufanikiwa kwa Arsenal kumpata
mchezaji wa kujaza nafasi yake.
Mchezaji waliyemtaka zaidi alikuwa winga wa Monaco Thomas Lemar ambayo inadaiwa alikataa kuhamia Arsenal.
Monaco walikuwa wamekubaliana na Arsenal kuhusu uhamisho wa Lemar, 21, ambaye huchezea timu ya taifa ya Ufaransa kwa £90m.
Sanchez alitaka kujiunga na Man City ambapo angeungana tena na kocha wake wa zamani alipokuwa Barcelona, Pep Guardiola.
Mchezaji
huyo wa Chile anatumikia mkataba wake wa mwisho katika klabu ya Arsenal na kuna
uwezekano mkubwa kwamba ataondoka majira yajayo ya joto bila kulipwa ada
yoyote.
Mchezaji aliyendoka katika klabu hiyo siku ya mwisho ni mshambuliaji Lucas Perez, ambaye alijiunga nao msimu uliopita kwa £17.1m. Perez
alirejea klabu yake ya awali Deportivo La Coruna kwa mkopo baada ya
kufunga mabao saba katika mechi 21 alizowachezea Gunners.
Kiungo wa kati wa Stoke Charlie Adam anasema kuwa, Arsenal wanamhitaji Alexis Sanchez zaidi ya wanavyohitaji £60m. Amesema bila ya kuwa na Alexis Snchez, Arsenal hawana nafasi ya kufuzu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kiungo wa kati wa zamani wa Aston Villa, Chelsea na Jamhuri ya Ireland Andy Townsend anasema: "Arsenal wako taabani. Ningemwacha Sanchez aende. Ishara alizoonyesha baada ya Arsenal kushindwa 4-0 na Liverpool hazikuwa nzuri. Amechoka na fikira zake ziko kwingine. Sidhani atayasahau yote na kurejea haraka kuwachezea kama kawaida"
Mwanachama wa bodi ya mashabiki, 'Arsenal Supporters' Trust Akhil Vyas anasema: "Naomba arudi tena kwenye timu na kujitolea kabisa, jambo ambalo hufanya akiwa uwanjani, kwa msimu huu. Dirisha
la usajili limefungwa kwa masikitiko, iwapo hatumnunui
mchezaji mwingine, basi ilikuwa lazima tusalie na Alexis"
Sanchez alichezea Arsenal mara ya kwanza msimu huu mechi waliyolazwa 4-0 na Liverpool Jumapili. Sanchez
alijiunga na Arsena kutoka Barcelona mwaka 2014 kwa ada ya takriban
£35m na alishinda kombe lake la pili ya FA akiwa na Arsenal mwishoni mwa
msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment